
Hayo yamesemwa
leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Mustafa
Abuod Jumbe wakati akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisi ya
Shirika la Meli Malindi Zanzibar.
Amesema upelekaji
wa meli katika chelezo ni suala la kawaida na halijaalishi kwa upya wa
mwaka mmoja au miwili ispokuwa ni maamuzi ya Shirika kufanya hivyo.
Amesema
wamepeleka chelezoni meli hiyo baada ya dhamana aliyotoa mtengenezaji ya
mwaka mmoja kumalizika, hivyo ilipaswa kuchunguzwa kabla ya dhamana
huyo kumalizika muda wake Disemba mwaka huu.
Aidha amesema
meli hiyo katika ukaguzi wake utakao fanywa nipamoja na kutia rangi
,ukaguzi wa viokozi ,mashine ukungu na mambo mengi yatayonekana
kurekebishwa.
Amesema gharama
ya matengenezo hayo yanatarajiwa kufikia dolazaidi ya 90 elfu ambapo
zitagawiwa thuluthi tatu ,thuluthi moja mjenzi wa meli na sehemu mbili
zilizo bakia zitatoa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Hata hivyo
aliwataka wananchi kuondosha hofu na wasiwasi kwa kuikosa meli hiyo kwa
kipindi kifupi na badala yake Shirika la Meli la Zanzibar limefanya
mazungumzo na uongozi wa meli ya seling ili kuhudumuia usafiri kwa muda
huo kwakwenda Pemba na Daresalaam mara tatu kwa wiki.
Pamoja na hayo
Katibu huyo aliwambia wandishi wahabari kua Serikali ina mpango wa
kununua meli mpya mbili ambayo moja itahudumia abiria pamoja na mizigo
na nyengine itakuwa meli ya mafuta.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
chanzo;zanzinews.
Comments