Wananchi wa Zanzibar wameshauriwa kutembelea sehemu za kihistoria
zilizopo nchini ili kujifunza historia ya nchi yao na kutuza utamaduni
iliopo.
Akizungumza na chanzo hiki cha habari msimamizi wa pango la
kihistoria la mwanamiza lililopo kizimkazi Ibarahim Naimu amesema
Zanzibar ni sehemu iliokusanya historia mbalimbali lakini wanashangwaza
na baadhi ya wazanzibar kutojuwa umuhimu wa historia hizo.
Hata hivyo amesema endapo wananchi watakuwa na utamaduni wa
kutembelea sehemu mbalimbali za kihistoria ikiwemo magofu ya zamani na
miskiti mikongwe watajifuza mambo mengi yatakayoibua vyanzo na kukuza
uchumi
Aidha ametowa wito kwa serikali kuunga mkono juhudi za watunza sehemu
hiyo ya kihistoria ya kizimkazi kwa lengo la kukuza sekta ya utalii na
kuimarisha ajira kwa vijana.
chanzo; zanzibar24.co.tz
Comments