Wananchi wa Vitongoji Pemba waitaka serekali kupitia upya tathmini ya fidia.

Serekali ya mapinduzi zanzibar imeombwa kupitia upya tadhmini ya wananchi wa kijiji cha vitongoji watakao vunjiwa nyumba zao kwa ajili ya ujenzi wa  Barbara unaondela.


Wananchi hao wameyasema hayo  huko kijijini kwao  wakati wakizungumza na mwandishi wa habari hizi juu ya kuwepo kwa malalamiko ya fidia waliaahidiwa kua ndogo  na  kutozingati thamani ya nyumba zao.


Ali Juma Khamis mmoja kati ya wananchi wa Vitongoji Vumba amefahamisha kua tathmini iliyofanywa ya kulipwa fidia hizo haikidhi mahitaji ikilinganishwa na garama za viwanja kwa sasa vimekua vya bei ya juu hasa kwa wananchi wenye kipato cha chini.


Amesema kuwa  ipo haja kwa serekali kuliangalia upya suala hilo  ili kuondokana na usumbufu ambao unaoweza kujitokeza.


 Nae Said Hassana Abdalla amesema jitihada za maksudi zinahitaji kwa serekali katika kutathmini upya gharama hizo  ili wapate sehemu za kuishi na familia zao bila kuwepo matatizo.


Kwaupande wake diwani wa wadi hiyo Abdalla Juma Abdalla emsema licha ya fidia kuwandogo lakini tatizo kubwa lililojitokeza nibaadhi ya nyumba ambazo zipo chini ya barabara, lakini hazipo kwenyempango wa kulipwa fidia haliambayo inaweza kuleta mgongano pale ambapo ujenzio huo utakapo endelea na kuleta madhara kwa nyumba hizo.


Amefahamisha kua wametoa elimu kwa jamii juu ya ujenzi wa barabara unavyo weza kuwanufaisha watu, lakini pia nachangamoto zinapojitokeza hususan kwa wale ambao ni wageni wa kijiji hicho huku akihimiza kulinda mila na tamaduzi za kijiji chao.


Sambamba nahyo sheha wa shehiya hiyo Salum Ayub Suleiman ameiomba wizara husika kuchukua hatua  za haraka kurudi kijijini hapo ilikujionea kero zilizopo kwa wananchi na kuhimiza kuwekwa matuta barabarani pindi itakapo kamilika ili kupunguza ajali zisiszo zalazima.

Comments