Wanafunzi wa vyuo wameiomba serikali ya Zanzibar kuwapatia elimu ya kujiajiri.

wanafunzi-wa-zitodWanafunzi wa vyuo wameiomba serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kuwapatia elimu ya kujiajiri wanapotoka vyuoni ili kuondokana na tatizo la ajira linalowakabili kwa mda mrefu.
Wakizungumza na Zanzibar24 Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha utalii Maruhubi  wamesema  wanapotoka vyuoni wanashindwa kujiajiri kutokana na kukosa elimu hiyo na kaulazimika kutegemea ajira za serikalini.
Wanafunzi hao wamesema pindipo serikali itaanzisha mikakati ya kuwapa elimu mara kwa mara kutasaidia kupunguza wimbi kubwa la vijana wasiokuwa na ajira mitaani .
Wakati huo huo akifungua mafunzo ya siku moja juu ya kuwajengea uelewa wa Ajira na Kujiajiri kwa wanafunzi hao Mkurugenzi  wa Idara ya Ajira Mmeri Ali Ameir amewahimiza wanafunzi  kufanya kazi kwa heshima na bidii ili kulingana na soko la ajira lilopo.
chanzo;zanzibar24.

Comments