Viongozi watatu wa serikali na meneja wa benki ya CRDB, wamefikishwa
mahakamani ya Bukoba kwa tuhuma za kula njama kwa kufungua akaunti za
bandia inayofanana na ile ya maafa ya waathirika wa tetemeko la ardhi
mkoani Kagera
Watumishi hao wamepandishwa kizimbani Alhamisi hii mkoani humo huku
wakikabiliwwa na mashtaka mawili ya kujipatia fedha kwa njia ya
udanganyifu na kufungua akaunti feki ya maafa Kagera yenye kesi namba
239/2016.
Waliopandishwa mahakamani ni pamoja na aliyekuwa ofisi tawala mkoa wa
Kagera (RAS) Amantius Msole na aliyekuwa mkurugenzi wa manispaa ya
Bukoba, Kelvin Makonda, aliyekuwa mhasibu mkoani Kagera Simbaufoo Swai
na meneja wa benki ya CRDB Kagera, Carlo Sendwa.
Wakili wa serikali Hashimu Ngole, alisema watuhumiwa hao wanashtakiwa
na makosa mawili, kushirikiana kufungua akaunti feki linalofanana na
akaunti ya maafa ya Kagera,na lingine ni kutumia vyeo na madaraka yao
kinyume na sheria.
chanzo;ubuyublog.
Comments