Wakulima Pemba waathiriwa na kiangazi.

Wakulima wa kilimo cha mboga mboga katika kijiji cha mkomani shehiya ya vitongoji  Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba wameiomba Serekali kuwafikishi huduma ya maji mashambani kwao ili kuendana na kilimo cha kisasa na kuondokana na kilomo cha kusubiria mvua.


Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi katika mashamba yao  mkomani shehia ya vitongoji wakulima hao wamesema wamekua wakizalisha bidhaa nyingi lakini wanashindwa kujiendeleza kutokana na ukosemu wa maji hali ambayo inarejesha nyuma harakati zao za kilimo.


Akizungumza kwaniamba ya wakulima wenzake Mariya Saleh Juma amesema  kilimo cha kusubiria nvua kimepitiwa na wakati kwani inaweza kupita miongo ambayo niyanvua na isinyeshe kabisa jambo ambalo linakatisha tama ya kuendeza kilimo hicho.


Amefahamisha kuwa licha ya kujaaliwa kuwa maziwa ya maji  lakini bado  wanapata usumbufu mkubwa wakuchota  kwa ndoo hadi mashambani jambo ambalo linawapotezea muda mkubwa, na kutofikia malengo walio jiwekea kwa haraka.


“laity kama tungalikua na mashine za kusukumia maji kutoka kwenye yale maziwa ingekua rahisi sana kwetu lakini yote yaha nikua hatuna vifaa, tunafanya tu ilikupata chochote ambacho kitatusaidia katika maisha yetu”.


Aidha amesema kuwa wamepata hasara kubwa ya kilimo chao cha matikiti, mabilingani, tungule, mabamia na mboga mboga nyengine  kuharibika  kutokana na kiangazi na kuwasababishia hasarakubwa.


Nae sheha wa shehiya hiyo Salum Ayub Suleiman amesema  ukosefu wa dhana za umwagiliaji maji mashambani kumesababisha hasarakubwa kwa wakulima  hususan  wa matikiti, mabilingani, tungule na mabamia kutohilimili ukame bila kupatiwa maji kwa wakati.


Amefahamisha kuwa  vikundivingi vya ushirika huanzishwa na badala yake kufa kutokana na ukosewu wa dhana za kujiendezea pamoja kukosa ruzuku hasa hasa kwa wakulima wadogo wadogo.


Nae diwani wa wadi ya Vitongoji Abdalla Juma Abdalla amesema kuwa kuwepo kwa ajira  zisizo rasmi zinachangiwa na hali ngumu za kimaisha lakini katika wadi  yao  tatizo hilo limepungua kwa asilimia kubwa.


Sambamba nayo ameiomba serekali kutoa mikipo kwa wajasiriamali wadogo wadogo ili waweze kujiendeleza na kuondokana na hali ngumu za kimaisha.


Comments