
Wajasiriamali
kisiwani Pemba wameshauriwa kubuni mbinu itakayoweza kuwasaidia
kuboresha thamani ya bidhaa wanazozalisha na kuwaletea pato
litakalowakwamua kiuchumi hapo baadae.
Wametakiwa
kujikita katika kujifunza njia ya usindikizaji wa mazao na uwekaji wa
vifungashio vinavyokubalika ili kuweza kuleta ushindani wa soko la
bidhaa la ndani na nje ya nchi .
Afisa
uchumi kutoka idara ya uwezeshaji wizara ya wanawake na watoto Pemba
Latifa Hassan Ali ameyasema hayo huko ukumbi wa uwanja wa Gombani Chake
chake Pemba katika mafunzo ya usindikizaji wa matunda na mboga mboga
kwa wajasiriamali kisiwani Pemba.
Amesema
changamoto inayowakabili wajasiriamali ni kukosa taaluma sahihi ya
uzalishaji na mashirikiano ya pamoja kitu kinachochelewesha kupatikana
kwa maendeleo endelevu miongoni mwao .
Nao
baadhi ya wajasiri amali hao wameitaka serikali kupitia wizara ya
uwezeshaji ,wazee , wanawake na watoto kuwatafutia mikopo ya mashine za
usindikizaji ili kuendana na kasi ya maendeleo ya uzalishaji mali
ulimwenguni ili bidhaa wanazozizalisha ziweze kupata soko kitaifa na
kimataifa .
chanzo;zanzinews.
Comments