Vyombo vya usalama vya shauriwa kutoa mafunzokwa Polisi Jamii.

askariSerikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia vyombo vya ulinzi na usalama imeshauriwa kuwapa mafunzo Polisi jamii wa shehia ya Kikungwi ili kujua njia rahisi za kuwakamata wahalifu.

Akizungumza na zanzibar 24 Mjumbe wa sheha  wa shehia hiyo Bahati Issa Suleiman amesema kuwa endapo wanajamii hao watapewa mafunzo wataweza kupambana na  watu wanaoendeleza vitendo viovu katika shehia hiyo.

Nao baadhi ya  wananchi wa Shehia hiyo  wamekiri kuwepo kwa tatizo hilo ambalo limekuwa ilikitia hofu wananchi wa oneo hilo hususani  nyakati za usiku.

chanzo; Zanzibar24

Comments