Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe Mohammed Aboud Mohammed
ameyasema hayo jana alipokuwa akijibu suali aliloulizwa na waandishi wa
habari kwenye mkutano wake na vyombo vya habari uliofanyika chake chake
kisiwani Pemba.
Katika suali lake
mwandishi wa habari Suleiman Rashid Omar alitaka kujua Serikali
inachukua hatua gani kuondoa upendeleo katika kutoa ajira kwa idara za
muungano ambazo wananchi kisiwani Pemba wanadai kwamba nafasi
zinazoletwa zinaporwa na kupewa vijana wanaotoka unguja.
Waziri Aboud
alisema serikali ya jamuhuri ya muungano imekua ikitoa nafasi za ajira
katika idara zake kwa mikoa yote ya Zanzibar, kila mkoa kufikisha majina
ya vijana ambao ni wakaazi wa mkoa huo na sio vyenginevyo.
Alifahamisha kua,
ajira zinazotangazwa ni chache na wanaojitokeza kuomba ni wengi hivyo
kunakuwako na uchambuzi wa kina katika kufanya maamuzi ya kuchagua
vijana wa kujiunga na idara hizo kwa kufikia vielelezo vya kila mmoja.
Aidha Waziri
Aboud alikiri kuwepo na idadi kubwa ya vijana wasio kuwa na ajira unguja
na pemba na kufahamisha kwamba serikali imeanza kuchukua hatua za
makusudi kulitafutia ufumbuzi swala hilo.
Alieleza kuwa
miongoni mwa mikakati hiyo iliyoandaliwa na serikali na ambayo imeanza
kutekelezwa ni kuahamasisha wawekezaji kuekeza katika sekta ya kilimo
,uvuvi na utalii ili vijana waweze kupata ajira na kupunguza ukali wa
maisha katika familia zao.
Aliongeza kuwa
kupitishwa kwa sheria mpya ya mafuta na gesi itafungua milango kwa
wawekezaji kuwekeza mitaji yao na hivyo kutoa fursa kwa vijana kupata
ajira pamoja na kupatikana soko la bidhaa la wajasiriamali wadogo
wadogo.
“kupitishwa kwa
sheria mpya ya mafuta na gesi kutafungua milango ya uwekezaji pamoja na
kuzalisha ajira kwa vijana na kutanuka soko la bidhaa za wajasiriamali
wadogo wadogo na wakati “alieleza.
Hivyo alisisitiza
kuwa serikali imepanga kuziendeleza fursa ambazo bado hazijatumika kwa
maslahi ya taifa kwa kuziboresha ili zilete tija kwa umma na taifa kwa
ujumla.
chanzo;zanzinews.
Comments