Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan alisema hayo jana wakati
akifungua Mkutano wa Mwaka wa Wataalamu wa Sekta ya Afya, wakiwamo
waganga wa mikoa na wilaya.
Awali akimkaribisha Makamu wa Rais, Mwenyekiti wa Waganga hao, Dk
Sudi Leonard katika risala, alisema kuna tatizo la ukosefu wa dawa na
vifaa tiba katika baadhi ya vituo vya afya nchini hali ambayo inazua
malalamiko kwa wananchi.
“Mheshimiwa Makamu wa Rais pamoja na mambo yote lakini tuna
changamoto ya ukosefu wa dawa na vifaa tiba hali hii imekuwa
ikisababisha malalamiko kwa wananchi. Mchakato wa upatikanaji wa dawa
pia umekuwa ukichukua muda mrefu kutoka MSD mpaka kufika sehemu husika
pia kuna hili kundi la watu maalumu na wao wanapokosa hulalamika,”
alisema Dk Leonard.
Akifafanua kuhusu juhudi za serikali kumaliza tatizo hilo, Makamu wa
Rais alisema fedha hizo zitanunua dawa, ambazo zitaenda moja kwa moja
katika vituo vya afya. Samia alisema, “tumetenga Shilingi bilioni 70 kwa
ajili ya kumaliza tatizo la dawa nchini pia tumetenga jumla ya Shilingi
bilioni 85 kwa ajili ya kupunguza deni MSD nia yetu ni kutaka huduma za
afya ziwe zenye ubora.”
Pamoja na utoaji wa fedha kwa ajili ya kuondoa tatizo hilo, Makamu wa
Rais alisema mpango wa muda mrefu wa serikali ni kuwa na kiwanda cha
dawa na kwamba mpango upo wa kujenga kiwanda hicho katika mkoa wa
Simiyu.
“Tuna maombi ya viwanda kama nane au tisa vya dawa na sasa
tunahangaika kufungua kiwanda kikubwa cha dawa katika mkoa wa Simiyu
lengo likiwa ni kukabiliana na tatizo la dawa pamoja na ile azma yetu ya
Tanzania ya Viwanda,” alisema.
Vilevile aliitaka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, kuhakikisha waganga wa tiba asili wote wanasajiliwa kutokana
na umuhimu wao katika jamii. “
Tiba mbadala na tiba asili ni taaluma yenye asili ya Kiafrika
tuliyorithi kutoka kwa mababu zetu kutokana na uhitaji wake mkubwa
ninaagiza wizara kuhakikisha waganga wa tiba asili wote wanasajiliwa na
wanafahamika,” alisema.
Aliwataka wataalamu hao wa afya, kutosita
kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wote wanaobainika kukiuka maadili
na viapo vyao vya kazi.
chanzo;habarileo.
Comments