Serikali ya Zanzibar imesema itaendelea kuunga mkono juhudi za UN.

serikaliSerikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kuunga mkono juhudi za Umoja wa kimataifa katika kusaidia sekta mbalimbali kisiwani Zanzibar ikiwemo kuboresha miradi ya kina mama katika kujikomboa na umaskini.
Akizungumza katika siku ya miaka 71 ya Umoja wa kimataifa UN huko mazizini Waziri wa kazi uwezeshaji Wazee,Vijana ,Wanawake na Watoto Zanzibar mordlin Castico amesema kwa kiasi kikubwa UN imekuwa mdau mkubwa wa maendelo katika kusaidia jamii.
Hata hivyo amesema malengo makuu ya serikali kupitia wizara hiyo ni kuwaandaa vijana  na wanawake juu ya kuwapa elimu ya kujiajiri na kupunguza kasi ya umaskini Nchini.
chanzo;zanzibar24

Comments