Polisi Mjini Magharibi wamshikila mhalifu wa kikundi cha Ubaya Ubaya.

download
Jeshi la polisi mkoa wa Mjini Magharib linamshikilia kijana mmoja anaedaiwa kuongoza genge la vijana linaloiba kwa kutumia mapanga.
Akizungumza na Zanzibar24 kamanda wa polisi wa mkoa huo Hassan Nassir amesema kijana huyo Mohamed Omar Haji mwenye umri wa miaka 20 mkaazi wa Fuoni alikamatwa maeneo ya Mwanakwerekwe.
Amesema kijana huyo amefanyiwa mahojiano na jeshi hilo na kutoa taarifa nyingi zinazoweza kusaidia kulingoa kundi la vijana hao wanaofanya vitendo vya uhalifu kwa kutumia mapanga.
Hivi karibuni jeshi la polisi mkoa wa Mjini Magharib liliwataka wananchi kushirikiana na jeshi hilo kwa kutoa taarifa za vijana wanaojishughulisha na vitendo vya wizi wa kutumia mapanga.
chanzo;ZANZIBAR24.

Comments