Ololosokwan yazindua utabibu kwa njia ya tehama.


201Katika uzinduzi wa mradi huo kwa ujumla wake, kliniki ndicho kitu ambacho kinaonekana kwenda karibu zaidi na wananchi wa Ololosokwan kwani itakuwa inatoa huduma za afya, bora za kisiasa na za haraka kwa wakazi wa kata za Soitsambu naa Oloipiri, Wilayani Ngorongoro.

Mradi mkubwa wa kijiji cha digitali cha Ololosokwan, Loliondo umezinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki, miaka miwili tangu kutiwa saini kwa uanzishwaji wake kati ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) na kampuni ya Samsung.
Hiki kitakuwa ni kijiji cha nne cha digitali barani Afrika cha kwanza kikiwa nchini Afrika Kusini huku kingine kikiwa Gabon na Ethiopia.
Kijiji hicho cha digitali ni nadharia ya Samsung katika kurejesha faida kwa umma na kina huduma mbalimbali ambazo zikiunganishwa na haja ya wananchi zitasaidia kubadili maisha ya wamasai na kuondokana na utegemezi wa mifugo pekee.
Uzinduzi rasmi wa kijiji hicho umefanywa na Mkuu wa mkoa Arusha Mrisho Gambo kwa niaba yaWaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu.
Kijiji hicho cha digitali kina shule yenye tehama ikiwa na maunganisho ya intaneti, kiliniki ya kisasa ikiwa na kituo cha teknolojia ya mawasiliano yenye kuwezesha utabibu (telemedicine) na jenereta linalotumia nguvu za jua.
Mradi huo ambao ulishuhudiwa utiaji saini na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Bi. Leah Kihimbi kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Dkt. N. Iriya kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) Dar es Salaam na wafanyakazi wa UNESCO mwaka 2014, kukamilika kwake kunawezesha UNESCO na serikali ya Tanzania kuwapatia wakazi wa eneo hilo huduma bora za afya na vijana wa Kimasai nafasi ya kupata elimu kutokana na ukweli kuwa kwa utamaduni na kazi zao za ufugaji wamekuwa wakipata shida ya kupata elimu.
Utiaji saini wake katika mwaka huo ulifanywa na Mkuu wa ofisi na Mwakilishi Shirika la UNESCO nchini Bi. Zulmira Rodrigues na Mkurugenzi wa Samsung Electronics nchini Tanzania, Bw. Mike Seo .
Kupitia kijiji hicho vijana wataendelea na masomo hata kama wanachunga mifugo yao kutokana na kupatiwa tablet ambazo zitawawezesha kujifunza hata wakiwa nje wakichunga mifugo yao.
Aidha miongoni mwa manufaa makubwa yatakayopatikana katika mradi huo wa kijiji cha digitali ni kuweza kupata nishati rahisi na iliyo rafiki kwa mazingira kwa kuwepo na jenereta linalotumia nishati ya jua.
Kuwepo kwa kijiji hicho kunataka kudhihirisha ni kwa namna gani teknolojia inaweza kutumika kuleta mabadiliko chanya yanayotakiwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi waliopo vijijini.
222Kijiji hicho cha Loliondo ambacho kitakuwa cha nne katika vijiji vya kidigitali barani Afrika kimeelezwa naMkuu wa mkoa wa Arusha Mheshimiwa Mrisho Gambo kama utekelezaji wa Sera ya Tiba Mtandao kutokana na kuzinduliwa kwa Kliniki Mtandao iliyopo katika Kijiji hicho.
chanzo;zanzibar24222

Comments