Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamanda Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam amesema kikosi hicho pia kimefanikiwa kukamata mtandao huo pamoja na kukomboa magari manne yaliyoibwa na watuhumiwa hao.
Amesema miongoni mwa watuhumiwa hao ni mwanafunzi wa chuo cha CBE aliyemtaja kwa jina la Dikson Valentino Godfrey (23) ambaye makazi yake ni Kimara.
Amewataja wengine kuwa ni Denis Ushaki(25), Alfred Ditriki(33) Venance Bureta(24).
Katika tukio lingine, Kamanda Sirro ameeleza kuwa, askari polisi walifanikiwa kukamata magari matatu ya wizi yaliyoibwa Dar es Salaam na kufichwa mkoani Arusha.
Amesema watuhumiwa wa mtandao huo wanashikiliwa Arusha na kwamba juhud za kuwafuata zinafanyika ili kujibu mashtaka yanayowakabili.
Hata hivyo, Kamanda Sirro amesema jeshi la polisi limekamata watuhumiwa 57 kwa makosa mbalimbali ikiwemo kuvunja nyumba usiku na kuiba, kuvuta na kuuza bangi, kunywa na kuuza gongo pamoja na vikundi vya panya road.
chanzo;zanzibar24
Comments