Waziri wa serekali ya mapinduzi zanzibar wakanusha ubovu wa mezani za kununulia karafuu Kisiwani Pemba.


Image result for zao la karafuu zanzibar

Waziri asiyekua  na wizara maalum wa serekali ya mapinduzi Zanzibar Said Sudi Said amewaomba wananchi wa Wilaya ya Mkoa kuondoa wasiwasi juu ya tatizo la mezani wanayopimiwa karafuu, kuwa ni mbovu na serekali itaendelea kutoa haki na hakuna mwananchi anaye ibiwa kwa njia yoyote.

Ameyasema hayo huko Mkoani alipokua akizungumza na wauzaji wa karafuu katika kituo cha ununuzi Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba.

Amesema kumekuwepo na uvumia kwa baadhi ya watu  kuwa mezani ya kupimia karafuu katika kituo cha kununulia karafuu mkoani ni mbovu, bali huwo ni uzushi unaolenga kuzoofisha ununuzi wa zao hilo na watahakikisha kua iwapo kuna mapungufu yoyote yanashughulikiwa.

Naye Waziri asiye na Wizara maaluum Juma Ali Khatib amewahakikishia wakulima wa zao la karafuu kuwa serekali haitowakopa wakulama katika mauzo ya zao hilo.

Amesema serekali inafedha za kutosha zinazo kimu kununulia zao hilo na wala haito shusha bei na kuahidi kuliendeleza kwa umakini mkubwa.


Sambamba nahayo mkuu wa uchukuzi wa kituo cha Mkoani Mohd Makame Haji  ( Pachingo ) amelalamikia shirika la meli ya Zanzibar kusababisha usumbufu wakati wa kupakia karafuu kwa ajili ya kusafirishwa.

Comments