Wananchi wa
kijiji cha kiziwani Shehia ya shungi Wilaya ya chake chake Pemba wameiomba
Mamlaka ya Maji Zanzibar(ZAWA) kufanya juhudi za kufikisha maji safi na
salama katika kijiji hicho iliyopatikana
kwa tabu hadi sasa .
akizungumza na zenj fm Mmoja ya awakaazi wa
kijiji hicho abeda Hamad amesema ni kipindi kirefu sasa wamekuwa wakipata
huduma hiyo kwa tabu na siku ambayo wanapata inakuwa hayakidhi haja kutokana na
kupatiwa ndoo 4 tu kwa kila baada ya siku mbili.
Kwa upande
wake bi Mwamize Khamis amesema huduma ya
maji safi na salama imekuwa ikipatikana
kwa tabu kadri ya miaka 25 hadi sasa.
Afisa
uhusiano Mamlaka ya Maji Pemba Suleiman Annas Massoud amesema sababu ya
kukosekana kwa huduma ya maji safi na salama katika baadhi ya vjiji ni kutokana
na mtandao wa kusambazia maji kuwa mdogo ila kwa sasa mamalaka ya maji Zanzibar
ZAWA imeshachimba visima 15 vitakavyoweza kueneza huduma ya maji safi na salama
katika vijiji vyote ambavyo huduma hiyo inapatikana kwa tabu na sio kwa kijiji
cha kiziwani pekee.
Hivyo
amewataka wananchi kisiwani pemba kuwa na subra katika kipindi hiki mamlaka ya
maji zanzibar ZAWA ikiwa ipo katika
juhudi na harakati za kufanikisha huduma ya maji safi na salama inawafikia
wananchi wa mjini na vijijini bila ya usumbufu wowote.
Comments