Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa limeshutumu vikali hatua ya Korea Kaskazini kufanya majaribio ya
makombora ya masafa marefu siku ya Jumatatu.
Pyongyang ilirusha
makombora matatu baharini mkutano wa viongozi wa mataifa 20 yenye
ushawishi mkubwa duniani ulipokuwa ukiendelea nchini China.
Kwenye azimio lililopitishwa kwa kauli moja na wanachama 15 wa baraza
hilo, ikiwemo China - mshirika mkuu wa Korea Kaskazini - baraza hilo
lilitishia kuchukua "hatua nyingine kali" dhidi ya taifa hilo
lisipositisha majaribio ya mabomu ya nyuklia na makombora.
Korea Kaskazini imezuiwa na UN kutekeleza majaribio hayo na imekuwa ikiwekewa vikwazo mara kwa mara.
chanzo;bbc.
Comments