Tamwa yapongeza JPM, Dk Shein.

CHAMA cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kinampongeza Rais John Magufuli na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kwa uteuzi wa viongozi na hasa wanawake.

Katika uteuzi uliofanyika karibuni wanachama kadha wa Tamwa walipata nafasi.

Tamwa iliwataja wanachama wake na nafasi zao ni Mahfoudha Alley Hamid (Ummie) ambaye amekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar, Maryam Hamdan (Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa na Sensa ya Filamu na Utamaduni Zanzibar), Nasra Mohamed Juma (Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) na Rahel Mhando (Katibu Tawala Wilaya mpya ya Kigamboni).

Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa, Eddah Sanga alisema taasisi hiyo inaamini kuwa, katika kuleta mabadiliko ya kimaendeleo nchini, uteuzi wa wanawake katika nafasi za juu ni fursa itakayowezesha kuondolewa kwa mapungufu yaliyopo kiuongozi ili kuwepo usawa na haki kwa watanzania wote.

chanzo;habarileo.

Comments