Assalamu alaykum
warahmatullah wabarakatuh.
Enyi watu,
Mcheni Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala). Na mjuwe ya kuwa hakika Mwenyezi
Mungu (Subhaanahu wa Taala) huumba atakavyo na huchagua atakavyo.
Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
قال
تعالى: (وَرَبُّكَ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ وَيَخْتَارُ مَا كَانَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ( {{Na Mola wako huumba
atakavyo na huchagua atakavyo, hawana viumbe hiari}}.. Na Mwenyezi Mungu
(Subhaanahu wa Taala) ndie anaye jua hekima kwa kila kitu anacho kichagua
miongoni mwa viumbe vyake.
Mwenyezi
Mungu (Subhaanahu wa Taala) huchagua Mitume miongoni mwa Malaika na watu. Na
Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) ameufadhilsha Mji wa Makka kushinda sehemu
nyingine. Na akauchagua Mji wa Madina kuwa ni mji aliohamia Mtume (Swalla Llahu
‘alayhi wasallam) na Masahaba.
Kisha
akauchagua Baytul Maqdis akajalia ni sehemu ya Mitume wengi ambayo Mwenyezi
Mungu (Subhaanahu wa Taala) ametuelezea habari zao katika Qur’an Tukufu. Na
Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) amefadhilisha baadhi ya Miezi kuliko mingine
na Usiku na Mchana. Akachagua Miezi mine Mitukufu (Dhul-qa’ada, Dhul-hijja,
Muharam na Rajab). Na bora wa masiku ni siku ya Ijumaa. Kwa hivyo, mtukuzeni
Allah (Subhaanahu wa Taala) na kumsifu na kumsalia Mtume Muhammad (Swalla Llahu
‘alayhi wasallam).
Hukumu ya
Swala ya Ijumaa
Swala ya
Ijumaa ni miongoni mwa swala muhimu za faradhi. Na sharia imetia mkazo zaidi na
kusisitiza kutekelezwa swala ya ijumaa kwa jamaa. Na malipo yake ni makubwa
zaidi.
Fadhila za
siku ya Ijumaa:
Kupata
Thawabu na Malipo kwa kila hatua ya kwenda Msikitini sawa na Mtu aliyesimama
kuswali na kufunga Mwaka mzima. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) :
[ Mwenye kuoga na kujisafisha, kisha akaenda Msikitini na mapema na akamkurubia
Khatibu na akasikiliza kwa utulivu.
Mwenyezi
Mungu (Subhaanahu wa Taala) atamlipa kwa kila hatua malipo sawa na Mtu
aliyesimama kuswali na kufunga Mwaka mzima] (Imepokewa na Ahmed).
Kusamehewa
Madhambi yake ya wiki mzima pamoja na siku tatu za ziada. Amesema Mtume (Swalla
Llahu ‘alayhi wasallam) : [ Mwenye kutawadha vizuri, kisha akaja Msikitini na
akamsikiliza Khatibu na kunyamaza. Anasemehewa Madhambi yake ya wiki mzima
pamoja na siku tatu]. Imepokewa na Muslim.
Kukubaliwa
dua katika siku hii tukufu. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) :
[Hakika katika Siku ya Ijumaa kuna wakati, haafikiwi Muislamu na wakati huo
hali akiwa anamuomba Allah, ila Mwenyezi Mungi humkubalia Dua yake].
Adabu na
Sunna za Siku ya Ijumaa:
Kuoga na
kujisafisha na kupaka manukato mazuri pamoja na kuondosha harufu mbaya
mwilini.. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) : [Mwenye kuoga siku ya
Ijumaa, kisha akaenda Msikitini na mapema. Mfano wake ni kama mtu aliyetowa
sadaka ya Ngamia].
Kwenda
Msikitini mapema na kumkurubia khatibu. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi
wasallam) : [Nedeni mkasali sala ya Ijumaa, na mkae karibu na khatibu].
Kujishughulisha
kwa Kumtaja Allah, kusoma Qur’an, kuomba msamaha, kuomba dua kwa wingi na
kumsalia Mtume Muhammad (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam).
Kumsilikiza
Khatibu kwa utulivu, bila ya kujishughulisha na mambo mengine. Asema Mtume
(Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) : [Mwenye kutawadha vizuri, kisha akaja
Msikitini na akamsikiliza Khatibu na kunyamaza. Anasemehewa Madhambi yake ya
wiki mzima pamoja na siku tatu]. Imepokewa na Muslim.
Mambo yalio
katazwa katika swala ya Ijumaa:
Kuja
Msikitini kuchelewa na kukata safu kwa kuruka watu, kwa lengo la kutaka kukaa
safu ya mbele. Siku moja Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) alimuona mtu
akikata safu na kuruka watu; Akamuambia kaa chini kwa hakika umewaudhi watu na
umefanya maasi makubwa.
Kuwashawishi
waja wa Mwenyezi Mungu, kwa kusoma Qur’an kwa sauti kubwa, au kufanya Dhikri
kwa sauti ya juu. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) aliwakataza Masahaba
kusoma kwa sauti ya juu, na akawambia; Asisome mmoja wenu Qura’n kwa sauti ya
juu kuliko mwingine.
Kuzungumza
wakati wa Khatibu anatoa khutbah ya Ijumaa. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi
wasallam) : [Ukimuambia mwenzako nyamaza na Khatibu akiwa anazungumza, kwa
hakika umeharibu swala ya Ijumaa].
Khatari ya
kuacha kuswali swala ya Ijumaa
Mtume
Muhammad amesisitiza na kutilia mkazo juu la suala la kutekeleza swala ya
Ijumaa. Na akawatahadharisha Waislamu wanaoacha kutekeleza swala hii.
Adhabu kubwa watakayo pata watu hao hapa
duniani ni nyoyo zao kuwa ngumu na kupigwa muhuri wa kughafilika.
Amesema
Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [ Hawataendelea watu kuacha swala ya
Ijumaa, mpaka Mwenyezi Mungu apige muhuri nyoyo zao, kisha watakuwa niwenye
kuishi katika mughafala].
Ndugu
Waislamu, tujihadhari sana na kuacha swala ya Ijumaa, kwasababu adhabu yake ni
nzito sana. Moyo ukiwa mgumu, basi mwanadamu anakuwa sawa na myama, hajali
lolote wala chochote. Utamuona hamuogopi Mwenyezi Mungu, kwa kufanya maasi
usiku na mchana.
Tunamuomba
Allah (Subhaanahu wa Taala) athibitishe nyoyo zetu juu ya twaa yake, na
atulinde na machafu yote.
Ndugu
Waislamu, katika Mafundisho ya Mtume Muhammad (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)
ni kuitukuza siku hii ya Ijumaa, kwani hii ni siku tukufu ilio chaguliwa na
Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) na kupatiwa Umma huu wa mwisho.
Mtume
Muhammad (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) alikhusisha baadhi ya vitendo katika
siku ya Ijumaa:
Kusoma Surat
Sijdah na Surat Insaan katika swala ya Al-Fajiri. Imepokewa na Abu Hureirah –
Radhi za Allah ziwe juu yake- {Alikuwa Mtume akisoma katika swala ya Al-Fajri
siku ya Ijumaa (Surat Sijdah) katika rakaa ya kwanza. Na katika rakaa ya pili
(Surat Insaan)} Muslim.
Kusoma Surat
Al-Kahfi. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): {Mwenye kusoma Surat
Al-Kahfi siku ya Ijumaa, Mwenyezi Mungu anampa mwangaza baina ya Ijumaa mpaka
Ijumaa nyingine}. Al-Bayhaqi na Haakim.
Kuzidisha
kwa wingi kumsalia Mtume Muhammad (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam). Amesema
Ibnu-Qayyim: “Mtume wa Mwenyezi Mungu ni Bwana wa viumbe vyote, na siku ya
Ijumaa ni bwana wa siku zote. Kumswalia Mtume siku hii ina malipo mengi
kushinda siku nyingine”.
Kuzidisha
kumuomba Allah (Subhaanahu wa Taala) katika siku hii. Kwasababu kuna wakati wa
kukubaliwa dua ya Muislamu. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) :
[Hakika katika Siku ya Ijumaa kuna wakati, haafikiwi Muislamu na wakati huo
hali akiwa anamuomba Allah, ila Mwenyezi Mungu humkubalia Dua yake].
Mwisho
Ndugu katika
Imani, kama tulivyo sikia umuhimu wa siku ya Ijumaa, na namna sheria ilivyo
tilia mkazo siku hii. Na vilivile malipo na thawaabu nyingi kwa Yule atakae
tekeleza ibada kwa masharti yake na nguzo zake. Ni jukumu letu kufanya bidii
kwa kufanya ibada mbali mabali kama alivyo tufundisha Mtume (Swalla Llahu
‘alayhi wasallam), ili tuweze kupata malipo na thawabu nyingi kutoka kwa Allah
(Subhaanahu wa Taala).
Enyi
Waislamu, Tushindaneni kufuata Sunna na Mafundisho ya Mtume (Swalla Llahu
‘alayhi wasallam) katika siku hii kuu.
Mwenyezi
Mungu atujaalie miongoni mwa waja wake wema na atupe uwezo wa kufuata Sunna za
Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam). Tunamuomba Allah atukubalie ibada zetu
na atupe mwisho mwema tukiondoka duniani.
Comments