Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Rais John Magufuli atakuwa wa mwisho kuhamia Dodoma na kupokewa na watumishi wa Serikali.
Rais
Magufuli akihutubia Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Julai 23 mwaka huu,
mkoani hapa alitoa tamko la Serikali kuhamia Dodoma ikiwa ni utekelezaji
wa uamuzi ulitolewa mwaka 1973.
Akizungumza
Jumatano wiki hii, katika kipindi cha Safari ya Dodoma kilichoandaliwa
na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Majaliwa alisema utaratibu wa
kuhama umepangwa kutekelezwa kwa awamu sita.
Alisema
awamu ya kwanza itaanza mwezi huu hadi Februari mwakani, ikiongozwa
naye, mawaziri wote, makatibu wakuu, naibu katibu mkuu na idara angalau
moja.
“Awamu
ya pili itaanza Machi hadi Agosti, 2017. Katika kipindi hicho makatibu
wakuu watapendekeza na kuomba fedha bungeni kwa ajili ya kazi hiyo,” alisema.
Kwa utaratibu wa Bunge, mikutano ya bajeti huanza Aprili hadi Julai ili kujadili na kuidhinisha mapato na matumizi ya Serikali ya mwaka mpya wa fedha.
Kwa utaratibu wa Bunge, mikutano ya bajeti huanza Aprili hadi Julai ili kujadili na kuidhinisha mapato na matumizi ya Serikali ya mwaka mpya wa fedha.
Majaliwa alisema awamu ya tatu itaanza Septemba hadi Februari, 2018 na zitaendelea nyingine, ya mwisho ikiwa mwaka 2020.
Akizungumzia
miundombinu, Majaliwa alisema Dodoma ina barabara za kutosha, nyingi
zikiwa za lami na hata zisizo za lami zinapitika vizuri.
Majaliwa
alisema kuna barabara ya kuunganisha mikoa mingine kama vile Singida,
Morogoro na Iringa, hivyo kuwafanya watu kuingia na kutoka mjini hapa
kwa urahisi. Kwa upande wa masoko, alisema yapo makubwa yenye vyakula
vya kutosha.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na
Walemavu), Jenista Mhagama hivi karibuni alisema ujenzi wa makazi, uzio
na ofisi binafsi za waziri mkuu umekamilika.
Mhagama
alisema kilichobaki ni kazi ya uboreshaji wa mandhari ya eneo la makazi
hayo yaliyoko Mlimwa, mjini hapa na barabara za kuunganisha kati ya
makazi hayo na nyingine kubwa.
Alimwagiza Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma, Jordan Rugimbana kuhakikisha mandhari ya eneo hilo yanaboreshwa ikiwa ni pamoja na kupanda maua.
Rugimba pia alipewa jukumu la kusimamia ujenzi wa barabara zinazounganisha makazi hayo na nyingine zilizopo maeneo hayo.
chanzo;mpekuziblog.
Comments