Ofisi ya Makamu wa Rais imekanusha taarifa inayosambazwa kwenye
mitandao ya kijamii kwamba Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan,
ameomba kujiuzulu nafasi yake.
Taarifa ya Ofisi ya Makamu wa Rais imesema taarifa hiyo ni ya uzushi na uongo haina ukweli wowote.
Imesema taarifa hiyo ni ya uchochezi inayolenga kuliweka Taifa kwenye taharuki.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Rais Mheshimiwa Makamu wa Rais yuko bega kwa
bega na Mheshimiwa Rais wa katika kufanya kazi zao kwa mujibu wa Katiba
ya nchi ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Ofisi ya Makamu wa Rais inawataka wananchi na Watanzania kwa ujumla
kupuuza taarifa hiyo ambayo inalenga kupotosha umma kuhusu ushirikiano
mzuri uliopo baina ya Viongozi hao.
Aidha Ofisi ya Makamu wa Rais inawasihi Watanzania kufanya kazi kwa
bidii na wajiepushe na vitendo vinavyolenga kuvuruga amani na utulivu
nchini.
chanzo;habarileo.
Comments