Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi, amewaasa
wasimamizi wa mitihani ya kumaliza elimu ya msingi kutofanya kazi kwa
mazoea ili kutoruhusu mianya itakayowafanya wanafunzi wasiokuwa na
uelewa kufaulu mitihani hiyo.
Alisema
kumekuwa na baadhi ya wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika wanafaulu
mithani hiyo kitendo kinachotia mashaka kwa wasimamizi hao kushindwa
kunyakazi waliyopewa kwa makini.
Mnasi
aliyasema hayo jana, wakati akitoa semina ya mafunzo kwa wasimamizi wa
halmashauri ya wilaya ya Ileje ambapo alisema usimamizi hafifu wa
mitihani umesababisha kuwepo kwa watumishi wasiokuwa na uwezo kitaaluma.
Aidha
kabla ya uteuzi wa Rais wa jamhuri ya muungazo wa tanzania Dr John
Pombe Magufuli mkurugenzi huyo ambaye kitaaluma ni mwalimu alikuwa afisa
elimu shule ya msingi manispaa ya iringa alisema iwapo ikibainika
kufaulu kwa wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika mtuhumiwa wa kwanza
kwenye uzembe huo atakuwa msimamizi wa mitihani na hatua kali
zitachukuliwa zidi yake.
“Nawatahadharisha
kwamba mnaweza mkarubuniwa kuwawezesha wanafunzi wasiokuwa na sifa
wafaulu mitihani hiyo,kufanya hivyo ni kukiuka kanuni za usimamizi na
uendeshaji wa mtihani na kuwaambia hayupo tayari kutumbuliwa na rais
kwasababu za wasimamizi”alisisitiza Mnasi.
Hata
hivyo Mnasi aliwataka wasimamizi hao kuwa makini katika kufanyakazi
hiyo na kama kuna jambo lolote ambalo hawajalielewa kuhusu kazi hiyo ni
vyema wakauliza ili kupewa majibu.
“hakikisheni
kuwa taratibu zote za mitihani zinazingatiwa ipasavyo na kuwataka
wasimamizi wote kufanya kazi yao kwa umakini na uadilifu wa hali ya
juu.“Nawaasa wasimamizi wa mitihani kujiepusha na vitendo vya
udanganyifu kwani serikali itachukua hatua kali kwa yeyote
atakayebainika kukiuka taratibu za mitihani,” alisema Mnasi.
Mnasi
alibainisha kuwa, serikali imezingatia uwezo wa kitaaluma, uadilifu na
uaminifu hivyo wasimamizi hao kupewa jukumu la kusimamia mitihani hiyo
muhimu ya kitaifa.
Aliongeza
kuwa mitihani hiyo ni muhimu ili kuliwezesha taifa kupima kiwango cha
elimu kilichpo nchini na kuwapata wasomi wa kiwango cha juu.
Nao
wasimamizi wa mitihani hiyo wamemuahidi mkurugenzi huyo kuwa
watasimamia mitihani hiyo kwa kufuata sheria na kanuni za usimamizi wa
mitihani walizopewa.
Mitihani
hiyo ya kuhitimu darasa la saba inatarajiwa kufanyika siku ya jumatano
tarehe 07 /09 /2016 na alhamisi tarehe 08 /09 /2016.
chanzo;mpekuziblog.
Comments