Jeshi la Magereza lawasilisha taarifa za utekelezaji wa sheria ya Bodi za Parole kwa Agustino Lyatonga Mrema.
Jeshi
la Magereza nchini limekabidhi rasmi ripoti ya taarifa ya utekelezaji
wa sheria ya bodi za Parole kwa Mwenyekiti wa bodi hiyo Taifa, Agustino
Lyatonga Mrema ikihusisha uelewa na elimu juu ya mambo ya Parole.
Tukio hilo limefanyika mapema leo Septemba 6.2016 katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi hilo la Magereza Jijini Dar es Salaam.
Kamishna
Jenerali wa Magereza ambaye pia ni Katibu wa Bodi ya Parole ya Taifa,
Bwana John Casmir Minja aliwasilisha taarifa hiyo ambapo imebeba maudhui
mbalimbali ikiwemo ya kujenga uelewa juu ya Parole kama sheria ya
Parole na utekelezaji wake.
Hii
ni pamoja na sifa za mfungwa wa Parole, muundo wa bodi ya taifa,
kitaifa na bodi za ngazi ya mikoa. Utendaji wa kazi kwa bodi ya Taifa ya
Parole na bodi za ngazi ya mikoa, mafanikio na changamoto ya bodi ya
Parole kitaifa na katika ngazi ya mikoa.
“Nimeipokea
taarifa yenu ya bodi ya Parole na mimi kama Mwenyekiti nitahakikisha
panapo tatizo tunasaidiana. Na yale magumu kama tatizo la bajeti ya
kuhakikisha Parole haikwami nitaiwasilisha mimi mwenyewe kwa Rais John
Pombe Magufuli” amesema Mrema
Ameongeza kuwa: “Kama
hakuna pesa tusitegemee miujiza kwa Parole kufanya kazi na hii ni
kutokana na ufinyu wa bajeti. Lakini labda tu nieleweshe jamii kwamba
nilipopewa kazi ya kuwa mwenyekiti wa bodi ya Parole ya Taifa watu
walidhani kwamba nakwenda magereza halafu nifungue milango wafungwa
watoke, Hapana si hivyo, hili jambo lina mchakato mkubwa na mrefu,” ameongeza Mrema
Aidha
Dkt.Mrema ametoa rai kwa jamii kuepuka kufanya uhalifu na kusema kuwa
Magereza si mahala pazuri kupeleka nguvu kazi ya Taifa
“Magereza
si mahala pazuri kwakweli, ni sehemu mbaya amabyo mtu anatakiwa aende
kwa bahati mbaya tu.la muhimu ni kuwa jamii iepukane na vitendo vya
uhalifu kwani nguvu kazi ya Taifa inapotelea jela”
Katika
suala lingine Dkt. Mrema amewataka wananchi hususani vijana kuachana na
makundi yanayohamasisha migomo na maandamano yasiyo na tija kwenye
Taifa
“Labda
tu niseme kwamba kufanya maandamano ya Lazima ni uhaini. Wenyewe
wanayaita maandamano yasiyo na kikomo, hayo ni uhaini niwaombe wananchi
wote hususani vijana waache kutumika na makundi yanayohamasisha
maandamano dhidi ya serikali na uongozi uliopo madarakani” amesema Mrema
..hivi
sasa mitaani kwetu kuna wafungwa watarajiwa wengi na mahabusu
watarajiwa wengi hvyo wazazi wakanyeni vijana wenu wasijihusishe na
vitendo vya uhalifu vitakavyowapelekea kwenda gerezani” amemalizia Dkt. Mrema.
Afisa
wa Jeshi la Magereza (aliyesimama kushoto) akisoma taarifa ya
utekelezaji wa sheria ya bodi ya parole kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole
Dkt. Augustine Mrema (wa kwanza kulia) wakati Mwenyekiti wa Bodi
alipomtembelea Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini ambaye pia
ni Katibu wa bodi ya Parole John Casmir Minja (katikati) mapema hii leo
jijini Dar es Salaam.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini ambaye pia ni Katibu wa bodi ya
Parole John Casmir Minja akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Dkt.
Augustine Mrema wakati alipomtembelea ofini kwake ili kujua matatizo
mbalimbali yanayoikabili bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Parole Dkt. Augustine Mrema akiagana na Kamishna Jenerali wa
Jeshi la Magereza Nchini ambaye pia ni Katibu wa bodi ya Parole John
Casmir Minja wakati Dkt. Mrema alipomtembelea ofisini kwake mapema hii
leo jijini Dar es Salaam. Picha na Eliphace Marwa
chanzo;mpekuziblog.
Comments