SHIRIKA la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) limeanza
zoezi la kuondoa mita za maji zote chakavu katika jiji la Dar es salaam
ili kupunguza tatizo la upotevu wa maji linaloendelea kulikumba shirika
hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Afisa
Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Cyprian Luhemeja amesema jumla ya mita
100,000 tayari zimeshaagizwa kwa ajili ya zoezi hilo.
“Tayari Dawasco ina mpango wa kubadilisha mita za Maji zote zenye
umri mkubwa kwenye maeneo yote ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na maeneo
ya mkoa wa Pwani, ila tutaanzia na maeneo ya Magomeni, Kawe pamoja na
Kinondoni kwa kuwa mita nyingi za maji huko zina umri wa zaidi ya miaka
10, “alisema Luhemeja.
Kwa habari zaidi usikose nakala yako ya Habarileo Septemba 7.
chanzo;habarileo.
Comments