Waziri wa Habari Nape Nnauye amevifungia vituo vya redio vya Magic FM na Redio 5 ya Arusha kwa madai ya uchochezi.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametangaza
kuvifungia kwa muda usiojulikana vituo vya Radio 5 ya Arusha na Magic FM
ya Dar es Salaam kwa sababu za uchochezi.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam, Waziri Nape amesema kuwa vituo hivyo kwa
nyakati tofauti vilitangaza habari ambazo ndani yake zina uchochezi.
“Adhabu
hii ya kuvifungia kwa muda vituo hivyo viwili inaanza leo (Agosti 29
2016) hadi pale kamati itakapomaliza kazi yake,” alisema Nape.
Aidha,
amesema kuwa ameiagiza Kamati ya Maudhui ya vyombo vya habari kuviita
vyombo hivyo na kuvihoji kwa kina kisha kumshauri hatua zaidi ya
kuchukua.
Waziri
huyo ameeleza kuwa Serikali inaendelea kutambua mchango mkubwa wa
vyombo vya habari katika kuleta amani na ushirikiano nchini na sio
vinginevyo.
Hivi
karibuni, Nape alitahadharisha kuwa vyombo vya habari vitakavyoripoti
taarifa ambazo ni za uchochezi vitakumbwa na rungu la kuhusika kwa
uchochezi pia.
chanzo;mpekuziblog.
Comments