Waziri wa biashara afanya uteuzi wa Wajumbe wa baraza la kusimamia mfumo wa utoaji leseni za biashara.
Waziri
wa Biashara, Viwanda na Masoko Mh. Amina Salum Ali kwa mujibu wa
sheria ya kusimamia mfumo wa Utoaji Leseni za Biashara Nam. 13 ya mwaka
2013 amewateua maafisa 12 kuwa wajumbe wa Baraza la kusimamia mfumo wa
utoaji leseni za Biashara Zanzibar.
Uteuzi
wa wajumbe wa kusimamia mfumo wa utoaji leseni za Biashara unafuatia
uteuzi wa Mwenyekiti wake uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhamed Shein.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Biashara,
Viwanda na Masoko wajumbe walioteuliwa ni Hussein Migoda Mataka kutoka
Wizara ya Fedha na Mipango, Ashura Mrisho Haji kutoka Wizara ya Habari,
Utalii Utamaduni na Michezo na Amour Ali Mussa kutoka Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Idara Maalum za Serikali.
Wengine
ni Hajar Idrisa Haji wa Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma
na Utawala Bora. Abeida Rashid Abdalla wa Baraza la Taifa la Watu Wenye
Ulemavu, Rashid Ali Salim Katibu Mtendaji Baraza la Kusimamia Mfumo wa
Utoaji Leseni za Biashara na Omar Said Shaaban kutoka Jumuiya ya
Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Wakulima (ZNCCIA)
Wajumbe
wengine wa Baraza hilo ni Khamis Salum Ali kutoka ZNCCIA, Mohamed
Salim Mohamed wa Jumuiya ya Watembeza Watalii (ZATO), Salmin Sharif
Khatib wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko, Abdulaziz Hamid Mahmoud
na Fatma Mussa Magimbi kutoka sekta binafsi.
Uteuzi huo umeanza tarehe 24 August 2016.
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
zanzinews.
Comments