Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Atembelea Kijiji Cha Katumba Wilayani Mpanda,azindua Mnara Uliojengwa Na Wakimbizi Waliopewa Uraia Wa Tanzania.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema kuwa wakimbizi waliopewa uraia wa Tanzania
na kuitumia vibaya nafasi hiyo kwa kuingiza watu wengine kinyume cha
sheria watanyang’anywa na kurudishwa walikotoka.
Aidha,
Waziri Mkuu amewaomba viongozi wa dini wawe wanawaelimisha waumuni wao
umuhimu wa kulinda amani na kuishi kwa kufuata sheria na taratibu za
nchi husika.
Kauli hiyo imetolewa jana
(Jumapili, Agosti 20, 2016) na Waziri Mkuu wakati akizungumza na
waliokuwa wakimbizi wa Burundi ambao kwa sasa wamepewa uraia wa Tanzania
wanaoishi katika Kata ya Katumba, Halmashauri ya Nsimbo wilayani
Mpanda.
“Wakimbizi
waliopewa uraia wameendelea kuingiza ndugu zao. Naagiza kamati ya
ulinzi na usalama ya mkoa ifanye ukaguzi katika kambi zote kwa sababu
zimegeuzwa kuwa maficho ya kuwahifadhi watu wanaoingia nchini bila ya
vibali,” alisema.
“Hakikisheni
mnachukua hatua kwa wote watakaoingiza watu kinyemela katika kambi za
wakimbizi za Mishamo na Katumba. Pia msiruhusu watu kuleta silaha kwenye
maeneo haya. Tanzania watu wanaoruhusiwa kutembea na silaha ni askari
tu,” alisisitiza.
Waziri Mkuu alisema
lazima ulinzi uimarishwe katika maeneo ya mipakani na wasipofanya hivyo
watu wengi wataingia nchini bila ya kuwa na vibali hivyo kusababisha
ongezeko kubwa la idadi ya watu.
Wakati
huo huo Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya
Mpanda wasiwaudhi wakulima na wafanyabiashara wadogo kwa kuwatoza
ushuru kwenye mazao wanapotoka shambani kama debe moja la nafaka na
wanaouza bidhaa ndogo ndogo.
“Mkulima
ametoka shambani na debe moja la mahindi unamtoza ushuru maana yake
nini? Halmashauri tusitafute mgogoro katika hili. Tafuteni biashara za
kutoza ushuru, mkulima anatoka kijiji cha Kanoge anakwenda kijiji cha
Ikongo ushuru wa nini?" Waziri Mkuu alihoji.
Waziri Mkuu alisema
“Tumewasisitiza mkusanye kodi lakini siyo hivyo. Mkiendelea kutoza
ushuru kwa wakulima wanaotoka shambani na mahindi kidogo mtasababisha
wakate tamaa ya kulima,”.
Alisema
wakimbizi 2,489 walichagua kurejea nchini kwao Burundi ila bado wapo
katika kambi hizo huku wengine 653 waliomba uraia lakini majina yao
hayakuonekana kwenye orodha ya waliokubaliwa wala kukataliwa uraia hivyo
mkoa unaendelea kufuatilia ili kujua hatma yao.
Mkuu
huyo wa mkoa alisema kuwa wakimbizi wengine sita walichagua kubaki
nchini lakini hawakuomba uraia, 398 waliomba uraia ila fomu zao
hazikukamilika,249 waliomba uraia ila majina yao hayakurudi huku wengine
973 hawakusajiliwa walipoingia nchini mwaka 2007/.2008.
IMETOLEWA NA:
JUMAPILI, AGOSTI 21, 2016.
chanzo;mpekuziblog.
Comments