Wanajumuiya ya Nocomped wahimizwa kuendeleza umoja wao.

Wanachama na wadau wa NOCOMPED COMMUNITY MEDIA  wametakiwa kuendeleza mashirikiano yao walio nayo ili kutekeleza vyema majukumu  ipasavyo.
Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa kamati ya usimamizi ya ujenzi wa kituo hicho ND. MOHD NASSOR SULEIMAN kilichopo Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati wa ziara maalum ya kukagua hali ya ujenzi na kuweka mikakati madhubuti ya kiutendaji ndani  ya jumuiya hiyo.
Amesema kila mmoja anatakiwa kua na ham ya kujitolea kwa moyo wote ili kutoa msukumo kwa viongozi wanaosimamia ujenzi wa kituo hicho cha radio na kukamilika kwa mudauliowekwa.
Amefahamisha kua bila ya kuwepo kwa umoja na mashirikiano dhati ndani ya jumuiya hiyo hakuna mafanikio yoyote ambayo yataweza kufikiwa na kurejesha nyuma maendeleo.
“ Nihakika penye umoja ndipo penye mafanikio umoja wenu ndio utakao kuza jumuiya pamoja na kuleta maendeleo endelevu katika kujikomboa kimaisha”.
“ siri ya maisha duniani nikua na maashirikiano bila ya mashirikiano hakiuna mafanikio hivyo bc tuamini yakwamba tutafanikiwa kwa mashirikiano yetu”.
Aidha ametoa wito kwa mashirika ya kisereli nayale ya umma kuunga mkojono jitihada za wananchi pamoja na jumuia ndogo ndogo kuzisaidia kwa hali na mali  ilikujikimu kimaisha na kuondokana na hali ya utegemezi.
Nao wadau wa jumuiya hiyo wamemuhakikishia mwenyekiti huyo kua  kwataendeleza kuyalinda mashirikiano yao ili kufikia pale ambapo wamelenga kupafika na kuondokana na hali ngumu ya kimaisha.
BAKAR HAMAD ABDALLA kwaniamba ya wadau wenzake amemuomba mwenyekiti huyo kuendelea kua na moyo wa subra kwa kuendelea kujitolea ili waweze kuyafikia kwa urahisi malengo ya ujenzi wa kituo hicho.
Amesema licha ya mafanikio yaliyo fikiwa na jumuiya hiyo  ipo haja kwa mwenyekiti huyo pamoja na wadau wengine kuendelea kujitolea,  kwani nguvu za ziada zinahitaji ili kukamilisha ujenzi wa kituo hicho cha radio.
“ Ipohaja kwa serekali na taasisi nyengine za umma kuungana kwa pamoja ili kukidhhi matwa na malengo tulio jiwekea ili tuweze kukamilisha vyema kituo chetu na malengo yetu yakamilike kwa muda muafaka”.

Comments