AMA kweli….. hawakukosea wahenga walivyonena ‘umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu’’.
Ukitaka maana yake, fikiria, kaa chini, tikisa akili na chemsha bongo lazima utapata jawabu.
Sio tatizo… kama hayo yote huyawezi, nifuate, njoo, nisome aya kwa aya, na kisha mstari mmoja baada ya mwengine, utajua tu.
Naanza
kukufamisha kwa dhati, hebu jaribu kumuua chawa kwa kutumia kidole
chako chochote kile kimoja, jaribu basi…..anza..twendee…haya muuwe…aaa
umeshindwa.
Sasa
changanya vidole vyako viwili na sasa muuwe chawa…haya twende mbona
imewezekana, maana hapo vidole vyako vilishirikiana na pale awali
ulivitenganisha.
Kauli
hii imefanikiwa sana Zanziabr na hasa kisiwani Pemba, baada ya viongozi
wa shehia, waratibu wao wa wanawake na watoto, Chama cha waandishi wa
habari Wanawake Tanzania TAMWA ofisi ya Zanzibar kushirikiana.
TAMWA
imekuwa haipati usingizi, kutokana na jamii ya Zanzibar na hasa
wanawake na watoto, kukumbwa na majanga ya ukatili wa kijinsia, ingawa
linapigwa vita lakini…..
Ndio
maana, TAMWA ikamua kuchanganya nguvu na wenzao wa serikali ya Denmark,
na kufanikiwa kupata mradi uliodumua kwa miaka miaka miwili, yaania
kuanzia 2012 hadi mwezi Septemba mwaka 2014.
Kwa
kiswa cha Pemba, mradi huu ulijitupa shehia sita za wilaya ya Wete,
ambapo pia iligundulika ndio shehia ambazo matendo ya ukatili wa kijnsia
kwa wanawake na watoto yamekithiri.
Hapo
TAMWA ikaanza kwa mafunzo, semina za hapa na pale, mbinu za kuibua
matendo hayo, na vikao vya kila mara, vilivyowashirikisha masheha
waratibu wao, maofisa kutoka ustawi na hata wizara husika.
“Lengo
la TAMWA la kuleta mradi huu kwenye shehia hizi, sio kwa upendeleo wala
kwamba chama hicho kinauhusiano na yoyote miongoni mwenu, ni kuwepo juu
matendo’’, alisema Mratib wa TAMWA Mzuri Issa akizungumza kwenye vikao.
Yeye
anaamini, utakapomalizika mradi huo wa ‘Kukuza Usawa wa Kijinsia na
Kuwawezesha Wanawake GEWE, matendo ya ukatili yawe yameshapungua.
Kabla
ya mradi huo, kuanza kwenye shehia za Kinyikani, Kiungoni, Shengejuu,
Mchangamdogo, Mjini ole na Kangani kulikuwa kukiripotiwa matendo 80 kwa
mwaka.
Wastani
wa kila shehia kwa matendo hayo ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na
watoto, likiwemo la ubakaji kabla ya kuanza kwa mradi wa GEWE, ni 13 kwa
mwaka.
Kwa
mfano, Sheha wa shehia ya Mchanga mdogo Asaa Makame Said anasema,
alikuwa akipokea malalamiko ya ukatili wa kijinsia sita, jambo ambalo
lilikuwa linatisha.
“Matendo
hayo ya ukatili wa kijinsia ni yale yaliokuwa yakiripotiwa na familia
tu kwangu, maana hata mbinu za kuibua ilikua hatuna’’, alisema sheha
huyo.
Hali
kama hii kabla ya kuingia kwa mradi wa GEWE, ilikuwepo shehia ya Mjini
Ole, ambapo Mratibu wa wanawake na watoto, Khadija Henop Maziku alikuwa
akipokea matendo 17.
“Kwa
kweli kabla ya TAMWA kutuletea mradi wa GEWE, matendo ya udhalilishaji
kwa wanawake na watoto yalikua juu sana, maana hata sisi waratibu na
masheha wetu hatukuwa wajanja wa kuyaibua”, anafafanua.
Zipo
pia shehia kama za Kinyikani ambapo uchunguuzi umebaina kuwa, kabla ya
kuingia na mradi huo, kulikuwa kukiripotiwa matendo 10 ambayo yalikuwa
yakiwadhalilisha wanawake na watoto kwa mwka.
Mratibu
wa mradi huo kutoka TAMWA, Asha Abdi Makame, yeye katika kipindi cha
mwaka 2013 wakati mradi huo ukiwa umeshapata mwaka mmoja, aliwataka
masheha kuhakikisha wanapunguza mtendoa hayo kwa kutoa elimu.
Kwa
wakati huo, Mratibu huyo, alisema lazima elimu wanayopewa kupitia vikao
vyao, wawaelimishe na wananchi wao, maana haitakuwa na maana mradi
ukimalizika kama hakuna mafanikio.
Hata Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya Wete Haroub Suleiman Hemed nae alisema anatarajia hasa katika shehia hizo sita, matendo ya udhalilisha baada ya mradi kumaliza yapungue.
Baada
ya kazi nzito iliofanywa na TAMWA, kwa kushirikiana na waratibuwa
shehia hizo sita, masheha, afisi ya ustawi na hata wizara inayosimamia
haki za wanawake na watoto, mradi umeongezwa na wafadhili.
Baada
ya wafadhili kuona kwamba mradi huu umesaidia sana katika kuyaibua na
kuyatokomeza matendo ya udhalilishaji wa kijinsia kwa kiasi kikubwa,
ndipo wakaamua kuuongezea muda, ambopo ulikuwa umemalizika mwaka 2014 na
sasa unakwenda hadi Disemba mwaka huu.
Hii
itaweza kuongeza nguvu zaidi kwa waratibu wa wanawake na watoto wa
shehia, katika kuyaibua matendo hayo, ambapo walifurahi sana na kusema
jitihada zitaendelea zaidi katika kuyatokomeza matendo hayo.
Waratibu
hao walisema wamefarajika sana kwa mradi huo kuongezewa muda, ambapo
utawafanya kujenga nguvu za pamoja katika kuyaondosha matendo ya ukatili
wa kijinsia.
Kwenye
kikao cha pamoja kilichofanyika Kiuyu Minungwini, mbele ya watendaji wa
TAMWA, masheha hao na waratibu walitakiwa sasa wafanya tathimini juu ya
mafanikio na changamoto.
Mwenyekiti
wa kikao hicho, sheha wa shehia ya Mjini ole, Khamis Shaaban,
aliinyanyua shehia moja baada ya nyengine ili kueleza mbele ya kikao
hicho kama kuna mafanikio ya mradi huo wa GEWE awali uliodumu miaka
miwili, ambapo sasa umeongezewa muda wa mwaka mmoja.
Mauwa
Said Khamis alikuwa wa mwanzo kutoa ripoti yake, ambapo alisema, kwanza
mradi umezaa matunda maana hata matendo ya ukatili awali yalikuwa 10,
ambapo kwa sasa anapokea matano (5) kwa mwaka.
“Mradi
wa GEWE kwenye shehia yangu, nasema umezaa matunda, maana kwa hesabu za
asilimia, sasa nnayo 0.41 kutoka asilimia 0.83 ya zamani kwa mwaka, kwa
matendo ya ukatili wa kijinsia’’, alisema.
Zamu
ya sheha wa shehia ya shengejuu Omra Faki Kombo, ikafika na kutakiwa na
kusema lolote na Mwenyekiti, akajilabu, kwa sasa anapokea matendo
matatu (3) kutoka saba (7) ya awali.
“Kabla
ya kuja mradi huu wa GEWE, hali ilikuwa ikitisha, maana yalikuwa
yakiripotiwa tu ni saba, lakini sasa nakaa hata miezi mitano bila ya
kujitokeza’’, alifafanua.
Mafanikio
makubwa hasa ya kujivunia kwa TAMWA ni kwenye shehia ya Kangagani,
ambayo kabla ya kufikiwa na mradi huu, Mratibu wake Awena Salim Kombo
alisema yalikua 30.
“Sasa
leo tukiwa mradi umeshakamilika kwa mwaka mzima napokea na kuibua
matendo 10, sawa na asilimia 0.83, kutoka wastani wa matendo 2 kwa
siku’’, alifafanua.
Kwenye
shehia pia ya Mchanga mdogo sheha wa shehia hiyo Asaa Makame Said, naye
anasema inagwa kwake huwa ni ya kujirudia rudia, lakini mafanikio yapo.
“Kama
naangalia mafanikio ya mtendo ya ukatili wa kijinsia, basi kwenye
shehia yangu nasema niko pazuri, maana sasa kwa mwaka napata matatu (3),
kutoka sita (6) kabla ya GEWE’’, alifafanua.
Afisa
ustawi wa Jamii wilaya ya Wete Haroub Suleiman Hemed, anasema kama
mradi huo wa ‘GEWE’ ungeaanza miaka kumi iliopita, basi hata shehia ya
Kiungoni isingelikuwa juu.
“Maana
Mratibu wa shehia hiyo Mchanga Said Hamad, anasema sasa anapokea
matendo sita (6), ambapo kabla ya mradi yalikuwa 10 kwa mwaka’’,
alifafanua
Waratibu
hao wanasema, sasa dunia inakoelekea utatuzi wa matendo hayo ni magumu,
maana wakosaji kama matendo ya ubkaji huwa ni ndugu na jamaa wa
akaribu.
Mkuu wa mkoa wa kaskazini Pemba, Omar Khamis Othuman yeye anasema jambo lililofanywa na TAMWA kupitia mradi wa GEWE sasa ni kuendelezwa.
“Mimi
naamini umoja na nguvu na utengano ni udhaifu, sasa kama kuna mashirika
mengine yanayoguswa kama ilivyokuwa TAMWA, basi matendo hayo
yatapungua’’, alisema.
Kwa ujumla mradi huo wa awali wa GEWE uliokuwa ukiendeshwa na TAMWA tokea mwaka 2012 na kumalizika mwezi septemba 2014, kwenye shehia hizo sita za wilaya wete, umezaa matunda maana matendo ya ukatilia yamepungua kutoka 80 hadi 34.
Baadhi
ya wananchi wa shehia hizo walisema, elimu imewafikia lakini kwa sasa,
baadhi ya mtendo hayo huwa magumu kupungua maana watendaji ni watu wa
karibu.
Idda
Haji Makame wa shehia ya Mchanga mdogo, yeye anasema kama baba, kaka,
au mjomba anambaka mtoto wake, kesi za aina hiyo huwa vigumu kumalizika.
Asha
Abdalla Haji wa shehia ya Kangagani yeye, anasema lazima jamii
ibadilike, na kuhakikisha wanatoa ushahidi mahakamani ili wakosaji
watiwe adabu kwa mujibu wa sheria.
“Sisi
wenyewe jamii pia wakati mwengine ni kikwazo kumaliza kesi za ukatili
wa kijinsia kwa wanawake na watoto, maana huwa wazito kutoa ushahidi
mahakamani’’, alifafanua.
Ingawa
masheha na waratibu hao walisema kwa sasa changamoto kubwa ni vyombo
vinavyosimamia haki, kutofanyaka kazi zao kwa umakini.
Walipendekeza
kuwa sasa vyombo vya sheria na hasa Polisi na Mahakama, kushibishwe
taaluma ya kutenda haki ili wakosaji wahukumiwe.
Mratibu
wa Mradi wa GEWE kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania ‘TGNP’ Matha Samwel,
yeye anasema suala la kumaliza metendo hayo lazima ushirikiano uwepo.
Aliekuwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA),
Bi Valerie Msoka, anasema mradi wa GEWE, umekuwa na mafanikio makubwa
kwa jamii katika kujitambua na kuibua vitendo vya Ukatili wa kijinsia.
Lakini
anafurahi zaidi kwamba hata vyombo vya habari, vyenyewe vimekuwa weledi
wa kutafutana kuibua vitendo hivyo zaidi na hasa baada ya uwepo wa
mradi.
Wilaya zilizofanyiwa utafiti huo ni wilaya za Wete Pemba, Magharibi
Unguja, Kusini kwa Unguja, Kisarawe (Pwani), Newala (Mtwara), Lindi
Vijijini (Lindi), Mvomero (Morogoro) na wilaya mbili za Kinondoni na
Ilala (Dar es Salaam).
TAMWA
inaendelea kuwashauri wakuu wa kata na shehia, kuendelea kupiga vita
matendo hayo, hata kama mradi huo umefikia ukiongoni, maana suala la
kutimiza wajibu wao halihitaji ufadhili
chanzo;zanzinews
Comments