Serikali ya Tanzania imewasilisha
ombi la kukata rufaa, uamuzi wa kihistoria nchini uliopinga ndoa za
watoto walio chini ya umri wa miaka 18.Mwezi uliopita mahakama kuu
iliamua kuwa sehemu za sheria ya ndoa mwaka 1971, iliyoruhusu wasichana
kuolewa wakiwa na umri wa hata miaka 14 ni kinyume na katiba.
Kundi
la kutetea haki za watoto "Msichana Initiative" iliwasilisha kesi hiyo
mahakamani. Taarifa hiyo ya kukata rufaa imewashtusha wengi Tanzania ,
wengi wakishindwa kuelewa ni kwanini mkuu wa sheria angetaka kugeuza
hukumu hiyo.
Mwezi uliopita mahakama kuu iliipa serikali muda wa
mwaka mmoja kurekebisha kosa hilo na kuweka umri wa miaka 18 kama umri
sahihi wa watu kufunga ndoa, kwa wote wasichana na wavulana nchini.
Awali sheria ya ndoa ya mwaka 1971 nchini Tanzania
imetaja kuwa wavulana wanapaswa kuoa wakiwana miaka 18 huku wasichana
wakiwa na umri wa miaka 15. Kesi hiyo iliwasilishwa na kundi la kutetea
haki za watoto Msichana Initiative, kupitia wakili Jebra Kambole.
Asilimia
37 ya wasichana walio na umri wa chini huolewa Tanzania. Wasichana
wenye umri wa hata miaka 14 huozwa kwa idhini ya wazazi. Na wengi wao
baadaye huripotiwa kukabiliwa na unyanyasaji nyumbani na hutengwa katika
jamii - wakikosa nafasi za kusoma na kuajiriwa.
Hivi karibuni
bunge lilikarabati kipengee cha sheria ya elimu na sasa ina sehemu
inayotoa hukumu ya kifungo cha miaka 30 gerezani au faini ya dola 2500
kwa wanaume wanaowapachika mimba au kuwaoa wasichana wa shule.
chanzo;bbc.
Comments