Nchini Senegal, watu kadhaa
wameandamana mjini Dakar kumuunga mkono mwanamke mmoja raia wa nchi hiyo
aliyekamatwa majuma machache yaliyopita na kushtakiwa kwa makosa ya
kumuua mke wa mwajiri wake huko Saudi Arabia.
Familia ya Mbayang Diop na wanaharakati wa haki za binaadam wanahofu huenda akanyongwa kwa mujibu wa sheria za Saudi Arabia.
Ripoti
ya kukamatwa kwa Mbayang Diop zilikuwa tayari kwenye vyombo vya habari
vya Senegal siku chache zilizopita.
lakini sasa wanaharakati wa masuala
ya haki za binaadam wameanzisha kampeni kwenye mitandao ya kijamii
wakisihi kumuokoa Mbayang, kampeni ambayo imekuwepo kwa kipindi cha saa
24 zilizopita, kabla ya mkutano wa jumatatu uliofanyika kwenye msikiti
mmoja wa katikati mwa mji wa Dakar.
Wanasiasa wanawake, wakiwemo
wale wanaotoka chama tawala na upinzani, pia wafuasi wa asasi za kiraia
na chama cha wafanyakazi wa majumbani walikutana kwa ajili ya kesi ya
binti wa miaka 22 , ambaye aliondoka Senegal baada ya kuahidiwa kuwa
atapata kazi nzuri inayolipa vizuri nchini Saudi Arabia.
Badala yake, kwa
mujibu wa kaka yake, binti huyo alikuwa akinyanyaswa, hivyo alimuua mke
wa mwajiri wake baada ya kulumbana.
Mamlaka ya mambo ya nje ya
Senegal imesema wanafuatilia kesi hiyo kwa karibu na kutangaza kuwa
Balozi wa Senegal nchini Saudi Arabia atakutana na Mbayang siku ya
jumatano gerezani anakoshikiliwa.
Wanaharakati wameomba huruma ya Serikali ya Senegal
ili iweze kuzungumza na mamlaka za Saudi Arabia ili binti huyo arudishwe
nchini mwake na kushtakiwa.
Hata hivyo mamlaka hazijasema hatua gani zitachukua.
Wanaharakati
wa haki za binaadam, waliripoti visa vya unyanyasaji wanavyofanyiwa
wafanya kazi wa ndani kutoka nchini Senegal walioko Saudi
Arabia,Lebanon,Morocco na Algeria.
chanzo;bbc.
Comments