Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein Awaapisha Viongozi Aliowateua Ikulu leo.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
leo amewaapisha Manaibu Makatibu Wakuu wawili ambao aliwateua hapo jana.
Katika
sherehe hiyo fupi iliyofanyika Ikulu, Mheshimiwa Rais alianza kwa
kumuapisha ndugu Hassan Khatib Hassan kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto anayeshughulikia
masuala ya Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto.
Shughuli
hiyo ya kiapo ilikamilika kwa Mheshimiwa Rais kumuapisha Kamishna
Msaidizi wa Vyuo vya Mafunzo (ACP) Sida Mohammed Himid kuwa Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Serikali za Mitaa, Tawala za Mikoa na Idara
Maalum za SMZ anayeshughulikia Idara Maalum za SMZ.
Sherehe
hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Spika wa Baraza la
Wawakilishi Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar
Mheshimiwa Omar Othman Makungu, Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi,
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mheshimiwa Said Hassan Said na Katibu wa
Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee .
Wengine
ni Mkuu wa Mkoa Mjini Maghribi Mheshimiwa Ayoub Mohamed Mahmoud, Kadhi
Mkuu wa Zanzibar sheikh Khamis Haji na Mstahiki Meya wa Manispaa ya
Zanzibar Mheshimiwa Khatib Abdulrahman Khatib.
chanzo;zanzinews
Comments