
Baadhi ya viongozi wa siasa wametoa ushauri huo akiwamo
Spika wa zamani wa Bunge, Pius Msekwa aliyezungumza katika Ukumbi wa
Idara ya Habari (Maelezo) akiwataka Watanzania kuacha kufuata mkumbo wa
kisiasa.
“Ni tabia ya Watanzania kushabikia mambo wasiyoyafahamu
ilimradi yanawafurahisha masikioni au machoni mwao, hata huko mitaani
wanakimbilia ngoma bila ya kujua inatokea wapi au inaelekea wapi. Hivyo
nawasihi wawe makini na mbinu za siasa zinazotumiwa na baadhi ya vyama
kwa kuwa nyingine zina madhara ndani yake,” amesema.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Msamaha kwa Wafungwa (Parole), Augustine Mrema amesema hakuna
haja ya kufanya maandamano hayo kwani hayana faida kwa Taifa kwa kuwa
wananchi wa kawaida ndio watakaoathirika.
chanzo;mpekuziblog.
Comments