MKURUGENZI
Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), Rashid Othman amestaafu rasmi
wadhifa huo, huku akitajwa kuwa miongoni mwa viongozi waliofanya kazi
nzuri wakiongoza taasisi hiyo nyeti.
Habari
za uhakika kutoka ndani ya serikali, zilizopatikana jijini Dar es
Salaam jana, zilisema kuwa Othman alistaafu rasmi wadhifa huo Agosti 19,
mwaka huu akiwa ameiongoza taasisi hiyo tangu Agosti 20, 2006 ikiwa ni
takribani miaka 10.
Kiongozi
huyo aliteuliwa na Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kuwa
Mkurugenzi Mkuu ili kuziba nafasi iliyoachwa na aliyekuwa Mkurugenzi
Mkuu wa wakati huo, Cornel Apson Mwang’onda.
Aliapishwa
Ikulu Dar es Salaam Agosti 21, 2006. Kabla ya uteuzi wake, Othman
alikuwa Mkuu wa Utawala na Utumishi wa Idara hiyo ya Usalama wa Taifa na
kufanya kazi nzuri, iliyochangia kumwezesha kuteuliwa kuwa Mkurugenzi
Mkuu.
Awali,
Othman alitakiwa kustaafu mwaka 2013 kwa mujibu wa sheria, lakini
aliendelea kuongezewa mkataba wa mwaka mmoja mmoja hadi alipokubaliwa
kustaafu rasmi Ijumaa iliyopita.
chanzo;mpekuziblog.
Comments