Mashindano ya uhamasishaji wa lugha ya kiarabu kwa walimu wa vyuo vya kiarabu vilivyo chini ya Taasisi ya Samail yamalizika vyema.

JUMLA ya Wanafunzi 1041 sawa na 41.85%, wamefaulu mitihani yao ya lugha ya Kiarabu, kati ya wanafunzi 2700 waliofanya mitihani hiyo iliyosimamiwa na Taasisi ya Samail Academy iliyopo Chake Chake Pemba.

Awali Wanafunzi 10935 kutoka Vyuo 105 vinavyosimamiwa na taasisi hiyo, ndio waliotarajiwa kufanya mitihani hiyo, lakini walishinbdwa kutokana na mchujo uliokuwepo na kupatikana idadi hiyo.


Akitoa ripoti ya mitihani msaidizi wa Taasisi ya Samail Academy, huko katika ofisi za taasisi hiyo, katika mashindano ya lugha ya Kiarabu kwa walimu 30, wanaosomesha vyuo vya Quran vilivyopo chini ya Samail, Shekh Said Abdalla Nassir, alisema lengo la mashindano hayo ni kuwapima uwezo walimu hao juu ya kufundisha lugha hiyo ya kiarabu.

Alisema mitihani hiyo iliyofanyika katika maeneo Tisa tafauti, huku ikisimamiwa na walimu na viongozi kutoka Samail Academy ili kupata wahitimu bora.

Aliyataja maeneo ambayo mitihani hiyo imefanyika ni Wingwi, Chake Chake, Wesha, Chanja Mjawiri, Pujini, Ukutini, Mtambile, Mkoani na Micheweni.

Alisema alama za mitihani hiyo iligawika katika makundi mbali mbali, ambapo wanafunzi 67 walipata alama A, 120 walipata alama B+, 436 walipata alama B na wanafunzi 418 walipata alama C, huku baadhi ya wanafunzi wakifutia matokeo yao kutokana na sababu za kutokuwa waaminifu wakati wa kufanya mitihani hiyo.

Akizungumza na walimu hao mara baada ya kumalizika kwa mshindano yahoo, mkagunzi wa Elimu kutoa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba, Mwalimu Amour Rashid Aliy, aliwataka walimu hao kuitumia vyema taaluma hiyo waliyopatiwa kwa kwenda kwuafundisha wanafunzi wao.

Alisema mwanafunzi mzuria anayehifadhi Qur-an na kuijuwa ipasavyo lugha ya Kiarabu, basi mwanafunzi huyo hufanya vyema hata katika masomo yake ya skuli za kawaida.
“Mwanafunzi anayehifadhi Qur-an hanatatizo katika masomo yake mengine, ni mwanafunzi anayekuwa bora zaidi darasani na familia yake”alisema.

Alisema taaluma hiyo walioyoipata ni taaluma adhimu, kwani wako walimu wengi wanaitaka nafasi hiyo, lakini hawakubahatika kuipata.

Hata hivyo aliipongeza taasisi hiyo ya Samail Academy kwa juhudi zao wanazozichukuwa katika kuwafundisha watoto lugha ya Kiarabu, huku akiwataka walimu hao kuwa karibu na watoto mayatima ili kuweza kupata Baraka kutoka kwa mungu.

Mapema Rais wa Taasisi ya Samail Academy Shekh Nassir Said Alrawaahy, alisema ufahamu wa lugha ya kiarabu kwa baadhi ya walimu ni mdogo sana, lakini taasisi yake itajitahidi kuhakikisha walimu wote wanaifahamu lugha hiyo.

Aliwataka walimu hao kujitahidi kuisoma kwa bidii lugha hiyo, ili kuweza kuwafundisha wanafunzi wao mambo mbali mbali waweze kukisoma vyema Qur-an.

Comments