
Kamishna wa
Polisi Zanzibar Hamdani Omari amesema hayo wakati alipokuwa akizungumza
na waandishi wa habari huko Makao Makuu ya Polisi Zanzibar kuhusu
usimamizi na wajibu wa Jeshi la Polisi katika usimamizi wa hakimiliki .
Amewataka
wananchi kuelewa kwamba kutoa kopi ,kuuza vinasa sauti na picha za
kieletroniki vikiwemo CD,DVD na vyenginevyo bila ya leseni ya
hakimiliki ni miongoni mwa makosa ya jinai.
Aidha alisema
kutumia hakimiliki biila ya ridhaa ya mwenye haki kama vile kurudufu
kusambasa na kuonyesha kazi kwa umma ama kuibadilisha kazi na kuwa kwa
mtindo mwengine ni kosa kwa mujibu ya sheria ya hakimiliki No. 14 ya
mwaka 2003.
Amesema
hakimiliki ni mali ya anaemiliki ,ni kazi yake inaestahili ulinzi kwani
kuitumia bila ya ridhaa ya mwenye haki ni kosa kisheria.
Katika kusimamia
sheria ya hakimiliki Jeshi la Polisi limetoa taaluma kwa askari wake
wakiwemo makamanda wa mikoa yote ya Zanzibar katika mwaka 2008 -2009
ofisi ilianzisha kikundi kazi cha hakimiliki .
Alieleza kuwa
jumla ya polisi 100 wa Unguja na Pemba walipatiwa mafunzo ya utambuzi wa
makosa ya hakimiliki kupitia mtalamu wa utambuzi wa jinai za hakimiliki
SP Omar Muwowo kutoka jeshi la polisi Zambia na Interpol.
Kamishna huyo
alieleza kuwa Jeshi la Polisi lilifanikiwa kupambana na uharamia wa
hakimiliki kwa kushirikiana na Afisi ya hakimiliki kufanya ukaguzi
katika maeneo yote ya Unguja na kukamata nakala haramu za vinasa sauti
na picha vya kielektroniki vikiwemo CD , DVD‘S na MP3 zenye uzito wa
tani mbili .
Aidha alisema nakala haramu hizo ziliangamizwa kwa kushirikiana na Idaraya Mazingira Zanzibar.
chanbzo;zanzinews.
Comments