Imesimuliwa kutoka kwa Abu Huraira-Radhi za M/Mungu zimshukie Juu yake -kutoka
Kwa Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani Amesema:-
(Siku iliyo kuwa bora katika masiku ambayo limechomoza jua ni siku ya ijumaa.
Kwa Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani Amesema:-
(Siku iliyo kuwa bora katika masiku ambayo limechomoza jua ni siku ya ijumaa.
Ndani ya siku hii aliumbwa Adam,na ndani ya siku hii aliingizwa peponi ,na ndani ya siku hii alitolewa peponi (na kushushwa ardhini),na wala hakito simama kiyama isipokuwa siku ya ijumaa) kama alivyosema Mtume , Hadithi imepokelewa na Muslim.
2.Siku ya ijumaa ni siku ya waumini kukusanyika katika swala ya pamoja,swala ambayo ina tofauti na swala tano,kwani swala hii hupendezwa zaidi kuswaliwa katika misikiti iliyo kuwa mikubwa yenye kukusanya idadi kubwa ya waumini na kufunga misikiti midogo kama hakutokuwa na uzito juu ya suala hilo.
3:Siku ya ijumaa kuna saa ambayo dua hujibiwa
Imesimuliwa kutoka kwa Abu Huraira-Radhi za M/Mungu zimshukie Juu yake - amesema:
Kasema Mjumbe (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani (Hakika siku ya ijumaa kuna saa ambayo hato iafiki mja muumini akawa kasimama akiswali na kuomba Allah kitu ,isipokuwa Allah atampatia mja huyu kile kitu alicho kiomba) Kama alivyosema Mtume Hadithi imepokelewa na Maimamu wawili Bukhari na Muslim.
Kutokana na hadithi na ushahidi mbali mbali , yaonesha rai yenye nguvu kuhusiana na saa hii ambayo hupokelewa dua ni kwamba saa hii yapatikana kati ya swala ya alaasiri na magharibi.
4.Sadaka ndani ya siku ya ijumaa ni bora kulikoni masiku mengine:
Kama ilivyokuja katika hadithi liyo pokelewa na Kaabu (Swadaka ndani ya siku ya ijumaa ni bora kulikoni swadaka katika masiku mengine).
Anasema imamu Ibun al Kayyim-rahimahu LLAH-"Na swadaka ndani ya siku ya ijumaa ukilinganisha na masiku ya wiki ni kama vile kutoa swadaka ndani ya mwezi mtukufu wa ramadhani ukilinganisha na miezi mingine"
5:Siku ya ijumaa ni sukukuu ya wiki
Kutokana na hivyo yapendeza kuoga na kuvaa nguo nzuri. Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani anasema:(Hakika siku hii{ya ijumaa}ni siku ya iddi {sikuku} aliyo ijaalia Allah kwa waislamu,yule atakayekuwa anaelekea kuswali kwa ajili ya swala ya ijumaa basi na aoge)yaani:Allah kaifanya siku hii ya ijumaa kuwa ni sikukuu kwa waislamu.
6:Siku ya ijumaa ni siku ambayo waja husamehewa madhambi
Imepokelewa kutoka kwa Salmani-radhi za M/Mungu ziwe juu yake-amesema:
Amesema Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani (Haogi mtu siku ya ijumaa,na akajitoharisha kadri ya uwezo wake katika kujitoharisha,na akajipaka mafuta yake ,au akagusa{ akajipulizia} manukato ya nyumbani kwake,kisha akatoka kuelekea msikitini,akawa si mwenye kufarikisha kati ya watu wawili,kisha akaswali rakaa alizo andikiwa{pangiwa} kuziswali,kisha akawa ni mwenye kutulia na kukaa kimya pindi anapo zungumza imamu{khatwibu},isipokuwa mja huyu husamehewa madhambi yaliyo kati ya ijumaa hiyo na ijumaa nyingine)kama alivyosema Mtume Hadithi imepokelewa na Bukhari.
Madhambi haya yanayo samehewa kati ya ijumaa na ijumaa nyingine ni madhambi madogo madogo,ama madhambi makubwa huitaji toba maalumu ya mja kwa kukaa na kutubia madhambi hayo makubwa,kama vile Kumshirikisha Allah,Kuuwa,Kuzini,kunywa pombe na mengineyo.Na kama dhambi aliyo ifanya ilikuwa ni kuiba mali ya mtu basi airudishe mali ile kwa wahusika.
Twamuomba Allah aturuzuku elimu yenye manufaa,na matendo mema.
Ewe Mola wetu zipokee Dua zetu ... Amiin
Comments