Maduka mengi yanayouza filamu katika eneo la Kariakoo jijini Dar es
Salaam, yamefungwa baada ya mamlaka ya mapato Tanzania, TRA kuwataka
wamiliki waoneshe mikataba ya usambazaji wa filamu hizo za nje.
Filamu hizo zinadaiwa kutolipiwa ushuru. Kwa mujibu taarifa ya Channel
10, baadhi ya maduka yamefunguliwa nusu huku wamiliki wakifanya biashara
kwa kuibia.
chanzo; ubuyublog.
Comments