Ukerewe. Ofisa afya na usafi wa mazingira wa Halmashauri ya
Wilaya ya Ukerewe Joseph Bulugu Joseph amesema kaya 3,982 wilayani humo
hazina vyoo.
Aliyasema hayo jana alipokuwa akikagua ujenzi wa vyoo bora na vya gharama nafuu katika Kijiji cha Lutare.
Alisema kijiji hicho kina jumla ya kaya 78,952, hivyo alitoa siku 60 kuanzia jana kaya hizo ziwe zimejenga vyoo vya kudumu.
Alisema idara yake iko kwenye kampeni ya kupambana na magonjwa ya mlipuko, kwa hali kama hiyo haitaweza kufanikiwa.
“Ukosefu wa vyoo katika wilaya hii umesababisha kuwapo mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kuanzia Septemba mwaka jana hadi Machi mwaka huu, watu 764 waliugua na 21 kati yao wamepoteza maisha,” alisema Bulugu.
Alisema wanatekelezaji pia awamu ya pili ya mradi wa kitaifa wa usafi wa mazingira unaohusisha wilaya 165 nchini.

chanzo; muungwana
Comments