Kumekuweko mashambulizi katika
viwanja vya makazi ya wakandarasi wa kigeni nje ya mji mkuu wa
Afghanistan, Kabul, karibu na kikosi cha anga nchini humo kilichoko
karibu na mji wa Bagram.
Gari lililokuwa limebeba vilipuzi,
linaarifiwa kuripuka katika eneo la karibu na upande wa lango la
kaskazini la viwanja hivyo, shambulio ambalo linafanana na lililotukia
miaka mitatu iliyopita.
Mara baada ya shambulio hilo tayari waasi
wa Taliban wametoa tamko la kukubali kuhusika na shambulio hilo, na
kwamba wapiganaji wao wamekuwa wakishambulia kuelekea katia vinja hivyo.
Mpaka sasa hakuna tamko lolote kutoka katika serikali ya Afghanstan na pia hakuna maelezo zaidi kuhusiana na majeruhi.
chanzo;bbc
Comments