
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba
Viongozi na Watendaji wa Taasisi na Mashirika ya Umma wana wajibu wa
kubadilika na kubuni mbinu zitakazowezesha kuongeza mapato kwa Taasisi
hizo kwa faida ya Taifa na Jamii kwa jumla.
Amesema
Serikali Kuu haiwezi kuleta maendeleo bila ya kuwa na vianzio madhubuti
ambavyo ni pamoja na ukusanyaji wa mapato yanayokusanywa kupitia
taasisi zilizopewa jukumu la kushughulikia makusanyo katika vianzio
mbali mbali.
Balozi
Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akizungumza na Wakurugenzi na
Mameneja wa Matawi ya Benki ya Watu wa Zanzibar { PBZ }, Shirika la
Bima { ZIC }, Shirika la Meli pamoja na Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar { ZSTC }
waliopo Tanzania Bara hapo katika jengo la Ofisi ya Uratibu wa shughuli
za SMZ Mtaa wa Magogoni Jijini Dar es salaam.
Mkutano
huo pia ulilenga kumtambulisha rasmi kwa Wakurugenzi hao Mkuu wa Ofisi
ya Uratibu wa shughuli za SMZ Mjini Dar es salaam Ndugu Issa Mlingoti
Ali aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein kushika wadhifa huo mpya.
Balozi
Seif alisema Taasisi na Mashirika yanayosimamia fedha lazima yaongeze
jitihada mara dufu katika ukusanyaji wa mapato ili kukidhi mahitaji na
matarajio ya Taifa kwa vile hali ya fedha sio nzuri katika kipindi
hichi.
Alisema
suala hili ni vyema likaenda sambamba na matumizi bora ya fedha za
Serikali na kuwataka Wakuu wa vitengo waendelee kusimamia vyema na kuwa
wakali kwa kuwadhibiti watendaji waliokosa uaminifu.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifahamisha kwamba wapo baadhi ya
watumishi wa Umma wanaoendelea kukosa uaminifu katika utekelezaji wa
majukumu yao ya kila siku na kuamua kujilimbikizia fedha na mali kinyume
na taratibu na imani za Dini wanazozifuata.
“
Tumekuwa tukishuhudia ndani ya mashirika na Taasisi zetu za Umma
kujichomoza Vijana wasio na maadili ya kazi na kuamuwa kujilimbikizia
mali na fedha katika kipindi kifupi tokea wapate ajira na kuwakuta
tayari wana uwezo wa kumiliki majumba na magari tofauti na kiwango
wanachokipata katika mishahara yao ya mwezi ”. Alionyesha kusikitishwa
kwake na tabia hiyo Balozi Seif.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kwamba Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar tayari imeshaanza na utaratibu wa kupunguza matumizi ya fedha
yasiyo ya lazima katika Taasisi zake kwa lengo la kupata nguvu ya
utekelezaji kwa yale mambo yasiyo ya msingi na muhimu.
Aliwapongeza
Viongozi na Watendaji wa Taasisi na Mashirika ya Umma yanayowajibika
Tanzania Bara kwa jitihada wanazochukuwa katika kutoa huduma kwa
Wananchi mbali mbali wa Tanzania sambamba na kukusanya mapato
yanayosaidia Taifa.
Nao
kwa upande wao Mameneja na Waguruigenzi hao wa Taasisi za SMZ zinazotoa
huduma upande wa Pili wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania walielezea
mafanikio na changamoto wanaopambana nazo katika utekelezaji wa majukumu
yao waliyopangiwa ya kila siku.
Meneja
wa Shirika la Bima la Zanzibar Tawi la Dar es salaam Ndugu Imam Ally
Makame alisema Uongozi wa Bodi ya Shirika hilo unaangalia maeneo ya
Mikoa tofauti Nchini Tanzania ili iwekeze miradi yake kwa lengo la
kujitanua katika kutoa huduma zao zinazokubalika na wateja mbali mbali.
Nd.
Imam alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba mapato
makubwa ya Bima yanayokusanywa na Shirika hilo yanapatikana katika
Mikoa mbali mbali Tanzania Bara.
Alisema
mafaniko hayo yamechangia kubuniwa mbinu za kuwasiliana na Taasisi
nyengine za Fedha Zanzibar na upande wa Bara katika kuangalia namna ya
kujenga jengo la kudumu litakalopunguza gharama kubwa zinazotumika kwa
kukodi majengo ya huduma.
Kwa
upande wake Menaja wa Benki ya Watu wa Zanzibar { PBZ }Tawi la Dar es
salaam Ndugu Mohammed Bakari alielezea kwamba Benki hiyo kwa sasa haina
mpango wowote wa kutaka kujenga majengo yake ya kudumu kwa upande wa
Tanzania Bara.
Nd.
Mohammed alisema hatua hiyo inakuja kutokana na sababu za Kibenki
kulazimika kujenga Majengo yao kwa kutumia Mfuko wa Benki husika jambo
ambalo kwa sasa nguvu zao wameamua kuendelea kuzielekeza katika biashara
zaidi kwenye majengo ya kukodi.
Meneja
wa Shirika la Meli Zanzibar Ndugu Salum Ahmad Vuai amemueleza Balozi
Seif kwamba Uongozi wa Taasisi hiyo uko katika harakati za kutaka
kujenga Jengo kubwa la ghirofa litakalokuwa Kitega uchumi cha shirika
hilo katika Mtaa wa Magomeni Mjini Dar es salaam.
Nd.
Ahmad alisema kinachoendelea kwa sasa ni Uongozi wa Shirika hilo
kutafuta hati miliki katika eneo hilo ili wapate uhakika wa kuanzisha
mradi huo baada ya kukamilika kwa mazungumzo na taasisi za fedha za
Zanzibar kwa hatua ya mashirikiano katika ujenzi huo.
chanzo;zanzinews
Comments