Watu 8 wauawa Misri, el Sisi ataka vikwazo dhidi ya Libya viondolewe.

Watu wenye silaha wamelishambulia basi moja lililokuwa na maafisa wa polisi katika eneo la Halwan, kusini mwa mji mkuu wa Misri, Cairo, na kuua watu wanane akiwemo afisa mmoja wa polisi.
Shirika la habari la Reuters limeinukuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri ikisema kuwa, watu wanne waliokuwa wamefunika nyuso zao walishuka katika lori moja, baada ya kulifungia njia basi hilo na kuanza kulishambulia kwa risasi.
Wakati huo huo Rais Abdul Fattah el Sisi wa Misri ametaka vikwazo vya silaha dhidi ya Libya viondolewe.
Shirika la habari la Sporting limemnukuu el Sisi akisema hayo jana wakati alipoonana na Faiz al Sarraj, mkuu wa Baraza la Uongozi la Libya ambaye pia ni Waziri Mkuu wa nchi hiyo na kusema kuwa, Misri inaiunga mkono kikamilifu serikali hiyo mpya ya Libya pamoja na juhudi za jeshi la nchi hiyo za kupambana na magaidi.
Vile vile ametaka vikwazo vya silaha ilivyowekewa Libya viondolewe ili serikali na jeshi la nchi hiyo liweze kukabiliana kikamilifu na vitendo vya uhalifu na kudumisha amani na usalama nchini humo.
chanz;parstoday

Comments