Samia atabiri utumbuaji majipu CCM.


Samia alitoa tahadhari hiyo jana wakati akizungumza kwenye semina ya viongozi wa CCM mkoani Dodoma ambayo ilijumuisha Wabunge, Madiwani na viongozi wa ngazi ya wilaya na mikoa.

Alisema anafahamu kuwa ndani ya chama hicho kuna watu sio wasafi ambao walisababisha CCM ikatumia nguvu kubwa wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka jana.

"Ndugu zangu mnasikia utumbuaji wa majibu, na yakitumbuliwa huko juu nyie huku chini mnashangilia, lakini nataka niwaambie majipu yale hayajatuota wa juu tu, tuna taarifa za kutosha majipu yale yapo mpaka kwenu CCM mpaka ngazi za chini", alisema Samia.

Alibainisha kuwa utumbuaji huo wa majipu ndani ya chama hicho utaenda ngazi kwa ngazi na atakayechelewa kutumbua jipu lillilo mbele yake atatumbuliwa yeye.

chanzo;darwaya.com

Comments