Makumi ya wapiganaji mamluki wa Saudi Arabia waangamizwa nchini Yemen.

Makumi ya wapiganaji mamluki wa Saudi Arabia wameangamizwa nchini Yemen wakati walipokuwa wakitaka kutekeleza shambulio katika mji wa Taiz kusini mwa Yemen.
Ripoti zaidi zinasema kuwa, mamluki hao wa Saudia waliangamizwa na vikosi vya wananchi wakati walipokuwa katika harakati za kutaka kufanya shambulio mkoani Taiz.
Mamluki hao walikuwa wamekiuka makubaliano ya usitiashaji vita na walikuwa na nia ya kufanya shambulio katika mkoa wa Taiz wakati walipoangamizwa na vikosi vya kujitolea vya wananchi, imesema taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na vikosi vya wananchi wa Yemen.
Aidha ndege za kijeshi za Saudia zinaripotiwa kukiuka makubaliano ya usitishaji vita huko nchini Yemen.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, hali ya kibinadamu nchini Yemen inaripotiwa kuzidi kuwa mbaya siku baada ya siku.
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetahadharisha kuwa, endapo kutafanyika uzembe katika kudhamini bajeti ya dharura kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa Yemen, mamilioni ya wananchi wa nchi hiyo watakuwa katika hatari ya kukabiliwa na maafa ya kibinadamu.
Ripoti zinaonesha kuwa, hadi sasa watu wasiopungua 9,400 wameshauawa na wengine zaidi ya 16,000 wamejeruhiwa tangu Saudia na washirika wake walipoanzisha mashambulio ya kijeshi dhidi ya Yemen mwezi Machi mwaka jana kwa lengo la kumrejesha madarakani kibaraka wa utawala wa Aal Saud, Rais wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kuitoroka nchi Abd Rabbuh Mansur Hadi.
chanzo;parstoday.

Comments