Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani aonyesha wasiwasi wake kuhusiana na hali ya Burundi.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani ameonyesha wasiwasi alionao kuhusiana na hali ya mambo nchini Burundi.
Papa Francis amesema kuwa, kuendelea mivutano ya ndani nchini Burundi na hatua za Ulaya za kutatua mgogoro huo kutazuia kufanyika mazungumzo baina ya serikali na wapinzani.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Dunia amebainisha kwamba, kuendelea hali inayotawala nchini Burundi itakuwa sababu ya nchi hiyo kuzidi kutumbukia katika vurugu na machafuko.
Amesema kuwa, hakuna ishara zozote za kuiondoa Burundi katika vurugu na machafuko.
Burundi ilitumbukia kwenye machafuko tangu mwezi Aprili 2015 baada ya chama tawala cha CNDD FDD kumuidhinisha Rais Pierre Nkurunziza kugombea urais kwa mara ya tatu mfululizo.
Mbali na wahanga hao, hadi hivi sasa wananchi laki mbili wa Burundi wamelazimika kukimbilia nchi jirani.
Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa zaidi ya watu 400 wameuawa na wengine karibu laki mbili na 60 elfu wamekuwa wakimbizi tangu nchi hiyo ilipotumbukia katika machafuko.
Machafuko ya Burundi yameifanya jamii ya kimataifa kuingiwa na wasiwasi wa uwezekano wa kutokea vita vya ndani endapo hatua za haraka hazitachukuliwa kwa ajili ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro huo.
chanzo;parstoday

Comments