Kundi la Ansaruddin limetangaza kuhusika na shambulio dhidi ya askari wa kimataifa wanaolinda amani kaskazini mwa Mali.
Jana kundi hilo lilitoa taarifa na kusema kuwa, ndilo lililowashambulia askari wa kimataifa katika eneo la Kidali la kaskazini mwa Mali, siku ya Jumatano.
Askari watano wa Umoja wa Mataifa waliuawa katika shambulio hilo na wengine watatu kujeruhiwa. Askari wote hao watano ni kutoka nchini Chad.
Shambulio hilo la siku ya Jumatano limefanyika baada ya lile la mwezi Februari mwaka huu ambalo lilikuwa baya zaidi kufanywa na wanamgambo wenye silaha dhidi ya askari wa kimataifa wa kulinda amani kaskazini mwa Mali.
Askari wa kofia buluu wa Umoja wa Mataifa maarufu kwa jina la MINUSMA wako nchini Mali tangu mwaka 2013 kwa ajili ya kusaidia juhudi za kuleta utulivu katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.
Hata hivyo askari hao wamekuwa wakishambuliwa mara kwa mara na makundi yenye misimamo mikali katika maeneo hayo.
chanzo;parstoday.
Comments