Wananchi katika vijiji vya Kiuyu mbuyuni pamoja na Maziwang’ombe wametakiwa kuzingatia kanuni za afya.
Na SHAABAN ALI
Wananchi katika vijiji vya Kiuyu mbuyuni pamoja na Maziwang’ombe wametakiwa kuzingatia kanuni za afya ya kudumisha usafi wa mazingira katika maeneo yao ikiwa ni juhudi moja wapo ya kupambana na maradhi ya kipindupindu yanayo wakabili katika maeneo yao.
Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya micheweni Abeid Juma Ali kwa nyakati tofauti wakati alipokuwa akizungumza na wazee wa vijiji hivyo lengo likiwa ni kupambana na ugonjwa huo hatari.
Amesema hali ya ugonjwa wa kipindupindu inaendelea kukua siku hadi siku katika maeneo hayo hutokana na jamii kutofata ipasavyo maelekezo wanayo pewa na wataalamu wa afya.
Abeid amesema kuwa wazee wana uwezo mkubwa wa kuzungumza na wananchi wa vijiji vyao na wakasikilizwa katika uzuiaji wa biashara za maji maji na vyakula katika kipindi hiki cha mripuko kitu ambacho kinasaidia kuenea kwa ugonjwa huo.
Amesema kuwa serikali inachukua jitihada za maksudi ili kuhakikisha wananchi wanaondokana na janga hilo ambalo limewakabili katika kipindi hiki.
Kwa upande wao wazee hao wamesema wamelipokea kwa mikono miwili suala hilo na watalifanyia kazi kama lilivo kusudiwa.
Comments