Wakulima wa karafuu pemba wapongezwa.

Na Shaaban Ali.
Mdhamini wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC)  Pemba Abdalla Ali Ussi amewapongeza wakulima wa zao la  karafuu wa Wilaya ya Mkoani kwa kurejesha fedha za mikopo kwa wakati .

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko Ofisini kwake Wete , amesema kuwa tofauti na Wilaya nyingine za Pemba ,   Wilaya ya Mkoani ndiyo Wilaya pekee iliyorejesha fedha zote za mkopo .

Amesema  Shirika lilitoa mikopo yenye thamani ya shilingi milioni  222.5 kwa wilaya zote za Pemba ambapo Shilingi milioni 39  zimetolewa kwa wakulima wa Karafuu wa Wilaya ya Mkoani .

Aidha mdhamini ameeleza kuwa kati ya fedha zilizotolewa mikopo na Shirika  , jumla ya shilingi milioni 159 zimerejeshwa ambapo Shirika bado linadaizaidi ya shilingi milioni 63.

Hata hivyo amewataka wakulima ambao bado hawajarejesha mikopo hiyo kuirejesha ili kutoa fursa kwa shirika kuwakopesha wakulima wengine .

Comments