MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amezitaka nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika kuanza utaratibu wa kuziweka alama silaha ndogo ndogo ili kufanikisha azma ya nchi hizo ya kudhibiti tatizo la kuzagaa kwa silaha haramu.
Samia alitoa kauli hiyo jana kwenye ufunguzi wa mkutano wa mawaziri wa nchi wanachama wa taasisi inayopambana na tatizo la silaha haramu katika nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika (RECSA) uliofanyika jana Jijini Arusha.
Alisema utaratibu huo utasaidia kuzitambua silaha hizo zinatoka nchi gani endapo zitakamatwa na kuziharibu zisizokuwa na alama ili zisirudi tena mikononi mwa wananchi na kubainisha kuwa Tanzania tayari imeanza zoezi hilo.
Makamu wa Rais aliueleza mkutano huo kuwa inakadiriwa silaha ndogo ndogo zipatazo milioni 875 zimezagaa duniani kote na kati ya hizo asilimia 75 zinamilikiwa na raia na kwamba zaidi ya milioni 100 ya silaha hizo zinapatikana Afrika.
chanzo;habarileo.
Comments