Nyumba moja yaezuliwa na upepo Pemba.

Upepo mkali uliovuma majira ya saa kumi jioni hadi  saa moja ucku umeezua paa la nyumba katika kijiji cha kiuyu mbuyuni mtaa wa titimiko karibu na  uwanja wa mpira katika wilaya ya Micheweni Mkoa wa kaskazini Pemba.Wakisimulia kutokea kwa tukio hilo wakaaazi wa eneo hilo wamesema upepo huo ulikua mkali na kushinwa kufanya chochote kama jitihada za uokozi.Wamefahamisha kua kuafuatia upepo uliovuma katika kijiji chao umesababisha hasara kwa kuezua paa la nyumba ya bw. Mandela Omar mkaazi wa eneo hiloWamesema hadi sasa hakuna kiongozi yoyote wa serekali aliejitokeza kujua kuangalia madhara yalio tokezea katika maeneo yao.Aidha wamesema mabati yalio ezuka yaligonga nyuzo ya umeme ambayo imeanguka na kupelekea mtaa huo kukosa huduma hiyo muhimu  bila kuathiri maisha ya watu walio kuwepo katika eneo hilo.

Comments